Robati Lawrence, O.Cart. (1485 hivi – Tyburn, 4 Mei 1535) alikuwa padri wa Uingereza, priori wa monasteri ya Wakartusi ya Beauvale[1][2].

Kifodini cha mapriori watatu Wakartusi.

Kwa kukiri imani ya mababu na kwa kukataa kiapo cha kumtii mfalme Henri VIII kama mkuu wa Kanisa Uingereza badala ya Papa[3] alinyongwa ila kabla hajafa alikatwa vipandevipande ambayo vilitundikwa sehemu mbalimbali za mji[4]. Pamoja naye waliuawa mapriori wawili wengine wa shirika hilo, Yohane Houghton na Augustino Webster, tena padri Richard Reynolds wa shirika la Mt. Birgita na paroko mwanajimbo Yohane Haile.

Alitangazwa mwenye heri na Papa Leo XIII tarehe 9 Desemba 1886 na mtakatifu tarehe 25 Oktoba 1970 na Papa Paulo VI.

Sikukuu yake huadhimishwa na Wakatoliki tarehe ya kifodini chake[5].

Tazama pia

hariri

Tanbihi

hariri
  1. "Saint Robert Lawrence", English Martyrs Parish
  2. Monks of Ramsgate. "Carthusian Martyrs". Book of Saints, 1921. CatholicSaints.Info. 29 September 2012
  3. ""History of Beauvale", The Beauvale Society". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2013-12-17. Iliwekwa mnamo 2021-05-03.
  4. Cranmer, Thomas (1833). The Remains of Thomas Cranmer, Archbishop of Canterbury. Oxford University Press.
  5. Martyrologium Romanum

Viungo vya nje

hariri
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.