Yohane Houghton

Wafiadini Wakatoliki

Yohane Houghton, O.Cart. (Essex[1], 1487 hivi – Tyburn, 4 Mei 1535) alikuwa padri wa Uingereza, priori wa monasteri ya Wakartusi ya London[2] na mkuu wa shirika hilo nchini.

Mt. Yohane alivyochorwa na Francisco Zurbarán.

Kwa kukataa kiapo cha kumtii mfalme Henri VIII kama mkuu wa Kanisa Uingereza badala ya Papa alinyongwa ila kabla hajafa alikatwa vipandevipande ambayo vilitundikwa sehemu mbalimbali za mji[3]. Pamoja naye waliuawa mapriori wawili wengine wa shirika hilo, Robati Lawrence na Augustino Webster, tena Richard Reynolds na Yohane Haile.

Alitangazwa mwenye heri na Papa Leo XIII tarehe 9 Desemba 1886 na mtakatifu tarehe 25 Oktoba 1970 na Papa Paulo VI[4].

Sikukuu yake huadhimishwa na Wakatoliki tarehe ya kifodini chake[5].

Tazama piaEdit

TanbihiEdit

MarejeoEdit

Viungo vya njeEdit

  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.