St. Pierre na Miquelon

(Elekezwa kutoka Saint Pierre and Miquelon)
Saint-Pierre et Miquelon
Bendera ya Saint-Pierre na Miquelon Nembo la Saint-Pierre na Miquelon
Wito: A mare labor (Kazi kutoka bahari)
Lugha rasmi Kifaransa
Mji Mkuu St. Pierre
Rais wa Halmashauri Kuu Stéphane Artano
Mkuu wa Mkoa (Préfet) Albert Dupuy
Eeno
 – Jumla
 – % maji

 242 km²
 0.0%
Idadi ya wakazi
 – Jumla (2011)

 6,080
Pesa Euro (€;EUR)
Jamla la pato la eneo
(Wanazaa kiasi gani cha mali kwa mwaka)
$48.3 Millioni
Kanda la saa UTC-3
Simu ya eneo 508 ¹
Intaneti TLD .pm
1. 0508 kutoka Ufaransa bara.

Saint-Pierre na Miquelon (kwa Kifaransa: Saint-Pierre-et-Miquelon) ni eneo la ng'ambo la Ufaransa (Collectivité d'outre mer) ambalo ni funguvisiwa karibu na pwani ya Kanada katika bahari ya Atlantiki.

Miquelon
Ramani
Mahali pa Saint-Pierre-et-Miquelon

Jiografia

hariri

Funguvisiwa liko karibu na jimbo la Newfoundland la Kanada.

Visiwa vikubwa zaidi ni Saint-Pierre (km² 26), Miquelon (km² 110), Langlade (km² 91) halafu kuna visiwa vingine vidogo . Miquelon na Langlade vilikuwa visiwa viwili lakini leo vimeungwa kwa kanda ya nchi kavu vyaitwa pamoja kama "Miquelon". Jumla la eneo ni km² 242 lenye wakazi 6,316 (Saint-Pierre: wakazi 5.618, Miquelon na Langlade: wakazi 698).

Karibu wote wanaongea Kifaransa na ni waamini wa Kanisa Katoliki.

Historia

hariri

Visiwa vimetembelewa na wavuvi kutoka Ulaya tangu karne ya 15.

Inaaminiwa ya kwamba makazi ya kwanza ya kudumu ya wavuvi Wafaransa yalianzishwa katika karne ya 17.

Tangu vita ya miaka saba visiwa hivi vilikuwa mabaki pekee ya koloni la Kanada ya Kifaransa.

Visiwa hii ni mabaki ya koloni kubwa la zamani lililoitwa "Nouvelle-France" (Ufaransa Mpya) na kuenea katika Kanada.

Uchumi

hariri

Uchumi umetegemea tangu mwanzo uvuvi. Siku hizi kuna pia utalii.

Wakazi wa visiwa ni raia wa Ufaransa. Huchagua bunge lao lenye watu 19. Bunge la eneo linamchagua mwakilishi mmoja katika bunge la kitaifa la Ufaransa.

Saint-Pierre na Miquelon si sehemu ya Eneo la forodha la Ulaya.

Viungo vya nje

hariri
 
WikiMedia Commons
  Makala hii kuhusu eneo fulani bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu eneo hilo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Je, unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.


Usitaje majina ya madiwani na viongozi au maafisa wengine wa sasa maana wanabadilika haraka mno.