Salome (mke wa Zebedayo)
Salome (kwa Kiebrania: שלומית, Shelomit, kutoka mzizi שָׁלוֹם, shalom, yaani amani[1]) alikuwa mke wa Zebedayo na mfuasi wa Yesu Kristo pamoja na wanae Yakobo Mkubwa na Mtume Yohane, waliokuwa marafiki wakuu wa Yesu pamoja na mtume Petro.
Kwa msingi huo alithubutu kumuomba Yesu awape wanae nafasi mbili za kwanza katika ufalme wake ujao.
Anatajwa kati ya wanawake waliosimama chini ya Yesu msalabani (Mk 15:40; Math 27:56) na kati ya wale waliowahi kwenda kaburini Jumapili asubuhi na mapema (Mk 16:1)[2].
Pengine anadhaniwa kuwa na undugu na Bikira Maria, mama wa Yesu.[3]
Picha
haririTazama pia
haririTanbihi
hariri- ↑ Behind the Name: Meaning, Origin and History of the Name Salome
- ↑ http://www.santiebeati.it/dettaglio/74850
- ↑ "NETBible:Salome".
- ↑ Martyrologium Romanum (Libreria Editrice Vaticana 2001 ISBN 88-209-7210-7
Viungo vya nje
haririWikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Salome (mke wa Zebedayo) kama habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |