Santo Domingo ni mji mkuu wa Jamhuri ya Dominikana. Ni kati ya miji ya kale kabisa ya Karibi: ilikuwa mji wa kwanza ulioanzishwa na Wahispania katika Amerika. Kuna majengo ya kwanza ya historia ya kikoloni katika Amerika yote yaani kanisa la kwanza, chuo kikuu cha kwanza na hospitali ya kwanza.

Santo Domingo

Santo Domingo ya kihistoria (Kanisa Kuu)
Habari za kimsingi
Utawala Wilaya ya Kitaifa (Distrito Nacional)
Anwani ya kijiografia Latitudo: 18°30′N - Longitudo: 69°59′W
Kimo 14 m juu ya UB
Eneo - 80 km²
Wakazi - mji: 913,540 (2001)
- rundiko la mji: 2,500,000
Msongamano wa watu watu 1,141 kwa km²
Simu +1809 (nchi yote)
Mahali

Idadi ya wakazi ni mnamo milioni mbili.

Wakati wa udikteta wa Rafael Trujillo mji uliitwa "Ciudad Trijillo" (mji wa Trujillo) kati ya miaka 1936 hadi 1961.

Historia hariri

Santo Domingo imekaliwa na Wahispania tangu mwaka 1496 ikaundwa kama mji mwaka 1498 na Bartolomeo Kolumbus (kaka ya Kristoforo Kolumbus) kwenye mdomo wa mto Ozama ikapewa jina "La Nueva Isabela" kwa heshima ya malkia ya Hispania. Ikaharibika na tufani mwaka 1502 na kujengwa upya upande wa magharibi wa mto.

Kanisa Kuu la Santa Maria de la Encarnación ni kanisa la kale la Amerika yote lilioanzishwa mwaka 1521 na kukamilika 1540. Hadi mwaka 1992 lilikuwa na kaburi ambalo kwa imani ya wenyeji lilikuwa la Kristoforo Kolumbus lililohamishwa kwa sherehe ya miaka 500 ya kufika kwake Amerika na kupelekwa katika jengo jipya.

Chuo Kikuu kikaanzishwa mjini mwaka 1538.

Mji wa Kale uliingizwa na UNESCO katika orodha ya "urithi wa dunia".

  Makala hii kuhusu maeneo ya Bahari ya Karibi bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Santo Domingo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.