Saturnini wa Karthago (askofu)

Saturnini wa Karthago (alifariki Roma, Italia, 250 hivi) alikuwa askofu wa Kanisa Katoliki katika mji wa Karthago (katika Tunisia ya leo).

Mahali panapotunza masalia yake katika kanisa lenye jina lake huko Roma, Italia.

Baada ya kuteswa nchini kwao katika dhuluma ya kaisari Decius alipelekwa uhamishoni Roma ambapo hatimaye aliuawa kwa kukatwa kichwa.

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu mfiadini.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 29 Novemba[1].

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.