Sekondinus ni mmoja wa mashahidi wa imani ya Kikristo waliouawa tarehe 7 Machi 203 mjini Karthago wakati wa dhuluma dhidi ya Wakristo chini ya serikali ya Kaisari Septimius Severus (193-211).

Kifodini cha Mt. Perpetua na wenzake katika vioo vya kanisa la Bikira Maria huko Vierzon (karne ya XIX).

Anaheshimiwa tangu kale kati ya watakatifu wafiadini pamoja na watakatifu Perpetua na Felista wanaojulikana zaidi kama mashahidi Wakristo wa Afrika ya Kaskazini.

Pamoja na akina mama hao vijana na wanaume wengine 3 walikamatwa pamoja na kutupwa jela. Jinsi ilivyokuwa kawaida walipewa nafasi ya kuachana na Ukristo lakini wote walisimama imara wakabatiwza gerezani.

Walihukumiwa adhabu ya kifo katika uwanja wa michezo mbele ya watu wengi. Hukumu ilitekelezwa kwa njia ya wanyamapori. Waliraruliwa na wanyama mbalimbali, wakamalizwa kwa upanga, isipokuwa yeye aliyefariki gerezani.

Sikukuu yao huadhimishwa tarehe ya kifodini chao[1].

Tazama pia

hariri

Tanbihi

hariri
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.