Felista Mtakatifu
Felista (kutoka Kilatini "Felicitas" - Heri ) ni mmoja wa mashahidi wa imani ya Kikristo waliouawa tarehe 7 Machi 203 mjini Karthago wakati wa dhuluma dhidi ya Wakristo chini ya serikali ya Kaisari Septimius Severus (193-211).
Anaheshimiwa kati ya watakatifu wafiadini wanaojulikana zaidi kama mashahidi Wakristo wa Afrika ya Kaskazini.
Mama huyo kijana anakumbukwa pamoja na rafiki yake mtakatifu Perpetua na wengine 4 wanaume tarehe ya kifodini chao[1].
Felista alikuwa kati ya watumwa wa familia ya Perpetua sawa na Revocatus. Pamoja nao na Saturninus alikuwa mmoja wa wanafunzi wa imani ya kikristo mjini Karthago waliojiandaa kubatizwa. Kundi lote likakamatwa pamoja na kutupwa jela. Jinsi ilivyokuwa kawaida walipewa nafasi ya kuachana na Ukristo lakini wote walisimama imara wakabatiwza gerezani. Felista alikuwa mjamzito mwenye uchungu wa kujifungua, hivyo kisheria angestahili kuachiliwa, kumbe alionekana mtulivu mbele ya wanyamapori.
Walihukumiwa adhabu ya kifo katika uwanja wa michezo mbele ya watu wengi. Hukumu ilitekelezwa kwa njia ya wanyamapori.
Matendo ya Perpetua na Felista
hariri"Matendo ya Perpetua na Felista" ni maandishi ya pekee kwa sababu kuna kumbukumbu ambazo zinasimulia habari zake gerezani na wataalamu huamini ya kwamba zimeandikwa na Perpetua mwenyewe (sura III-X). Kama hii ni kweli, ni maandiko ya kale kabisa ya mwanamke Mkristo katika historia iliyotunzwa.
Tazama pia
haririTanbihi
haririFilamu
hariri- Perpetua: Early Church Martyr (2009) - documentary.
- Torchlighters: The Perpetua Story (2009) - animated DVD for children ages 8–12.
Viungo vya nje
hariri- "Matendo ya Mt. Perpetua" kwa Kilatini, Kigiriki na Kiingereza. Kitabu chote katika www.earlychurchtexts.com.
- "Matendo ya Perpetua na Felista" katika tafsiri ya Kiingereza.
- Medieval Sourcebook: The Passion of Saints Perpetua and Felicity. Ilihifadhiwa 6 Machi 2011 kwenye Wayback Machine. From W.H. Shewring, trans. The Passion of Perpetua and Felicity, (London: 1931), modernized.
- Henry Wace, A Dictionary of Christian Biography and Literature to the End of the Sixth Century A.D. 1911
- Patron Saints Index: St. Felicity Ilihifadhiwa 12 Julai 2011 kwenye Wayback Machine.
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |