Serafino wa Sarov
Serafino wa Sarov (kwa Kirusi Серафим Саровский, awali aliitwa Prokhor Moshnin (Прохор Мошнин), 19 Julai 1754 au 1759 - 2 Januari 1833) ni kati ya wamonaki maarufu zaidi wa Urusi kutokana na utakatifu wake.
Alistawisha mafundisho ya kimonaki kuhusu sala hasa na kujikana akayaeneza kwa walei.
Kwake lengo la maisha ya Kikristo ni kumpata Roho Mtakatifu zaidi na zaidi. Moja kati ya madondoo yake maarufu zaidi ni hili: "Jipatie roho iliyotulia, na maelfu ya watu wataokolewa kandokando yako."
Serafino alitangazwa mtakatifu wa Kanisa la Kiorthodoksi la Kirusi tarehe 19 Julai 1903. Hata Papa Yohane Paulo II alimzungumzia kwa kukubali sifa hiyo.[1]
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 2 Januari, lakini pia 19 Julai.
Maisha
haririMtoto wa Isidore and Agathia Moshnin, walioishi huko Kursk, Russia, baba yake alikuwa mfanyabiashara, lakini kazi hiyo haikumvutia.
Kadiri ya mapokeo ya Waorthodoksi, picha takatifu ya Bikira Maria wa Kursk ilimponya akiwa kijana. Baadaye alijaliwa njozi kadhaa.
Mwaka 1777, akiwa na umri wa miaka 19, alijiunga na monasteri ya Sarov kama mnovisi (poslushnik).
Mwaka 1786 alinyolewa kama ishara ya kuwekwa wakfu akapewa jina la Seraphim ("mwenye kuwaka" kwa Kiebrania). Baadaye kidogo alipewa daraja takatifu ya ushemasi.
Mwaka 1793 alipata upadrisho na kufanywa kiongozi wa konventi ya Diveyevo, lakini punde tu akawa mkaapweke kwa miaka 25.
Siku moja, akiwa anaokota kuni, Serafino alishambuliwa na wezi waliompiga kikatili wakitumia shoka alilowapa hadi akaachwa kama amekufa. Tangu hapo Serafino akawa mlemavu wa mgongo, lakini mahakamani alidai kwa nguvu wezi waachiliwe.
Hata hivyo, baada ya hapo alitumia usiku kucha mara 1,000 mfululizo akisali mikono juu kuelekea mbinguni.
Mwaka 1815, akitaka kutii njozi ya Bikira Maria aliyojaliwa, Serafino alianza kupokea waamini kwa sakramenti ya kitubio. Kwa muda mfupi alijulikana sana kutokana na karama zake za uponyaji na unabii. Kila siku alitembelewa na mamia ya watu, waliovutiwa na uwezo wake wa kujibu maswali yao kabla hawajamuuliza.
Ingawa Serafino alikuwa mgumu sana kwake mwenyewe, alikuwa mpole kwa wengine — akiwapokea mara nyingi kwa kusujudu,kuwapa busu la amani na kuwasalimu, "Kristo amefufuka!", akimuita kila mmoja, "Furaha yangu."
Alifariki amepiga magoti mbele ya picha takatifu ya Theotokos akiwa na umri wa miaka 74.
Tazama pia
haririTanbihi
hariri- ↑ Pope John Paul II, Crossing the Threshold of Hope, (Knopf, 1995), ISBN 978-0-679-76561-5, page 18.
Marejeo
hariri- Dmitri Mereschkowski et al. Der letzte Heilige - Seraphim von Sarow und die russische Religiosität. Stuttgart 1994
- Archimandrite Lazarus Moore: St. Seraphim of Sarov - a Spiritual Biography. Blanco (Texas) 1994.
- Michaela-Josefa Hutt: Der heilige Seraphim von Sarow, Jestetten 2002, Miriam-Verlag, ISBN 978-3-87449-312-3
- Igor Smolitsch: Leben und Lehre der Starzen. Freiburg 2004
- Metropolit Seraphim: Die Ostkirche. Stuttgart 1950, pp. 282 ff.
- Paul Evdokimov: "Saint Seraphim of Sarow", in: The Ecumenical Review, April 1963
- Iwan Tschetwerikow: "Das Starzentum", in: Ev. Jahresbriefe; 1951/52, pp. 190 ff.
- Claire Louise Claus: "Die russischen Frauenklöster um die Wende des 18. Jahrhunderts", in: Kirche im Osten, Band IV, 1961.
- Bezirksrichter Nikolai Alexandrowitsch Motowilow: Die Unterweisungen des Seraphim von Sarow. Sergijew Possad 1914 (in Russian)
- Bishop Alexander (Mileant), "Saint Seraphim of Sarov", Orthodoxy and the world, December 2007.
Viungo vya nje
hariri- St. Seraphim article on OrthodoxWiki
- St. Seraphim of Sarov life, writings and icons Ilihifadhiwa 14 Mei 2015 kwenye Wayback Machine. on Kursk Root (Korennaya) Icon Hermitage of the Birth of the Holy Theotokos site
- On the Acquisition of the Holy Spirit Spiritual conversation of Saint Seraphim
- A wonderful revelation to the world, www.stseraphim.org
- Uncovering of the relics of the Venerable Seraphim of Sarov Orthodox icon and synaxarion
- Glorification of Saint Seraphim. Sarov, 1903
- Photos of St. Seraphim glorification solemnity in Sarov (1903) Ilihifadhiwa 30 Machi 2012 kwenye Wayback Machine., Martha and Mary Convent site
- Photos of St. Seraphim glorification in Sarov (high res images), sarov.net
- St. Seraphim's biography Ilihifadhiwa 27 Septemba 2011 kwenye Wayback Machine. by Archimandrite Nektarios Serfes
- Portal devoted to 100-th anniversary of St. Seraphim of Sarov glorification Ilihifadhiwa 25 Novemba 2014 kwenye Wayback Machine. (in Russian)
- English page on Sarov monastery web-site
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |