Shemasi

(Elekezwa kutoka Ushemasi)

Shemasi ni kiongozi wa Kanisa anayeunganisha wenye daraja za juu na walei. Ushemasi ni daraja ya tatu na ya mwisho katika Kanisa Katoliki na madhehebu mengine kadhaa. Unatolewa na Askofu kwa kumwekea mtu mikono na kumuombea ili atoe huduma ya Neno la Mungu, ya liturujia na ya upendo. Unaweza kutolewa kwa namna ya kudumu au kama hatua ya kuelekea daraja ya upadri.