Siasa ya Malawi

(Elekezwa kutoka Siasa Nchini Malawi)

Siasa ya Malawi ina muundo wa taifa lenye demokrasia ya uwakilishi na mfumo wa urais. Rais wa Malawi ndiye kiongozi wa nchi na mkuu wa serikali.

Malawi

Makala hii imepangwa kwa mfululizo:
Siasa na serikali ya
Malawi



Nchi zingine · Atlasi


Mfumo wa uchaguzi unaotumika ni ule wa vyama vingi. Mamlaka ya Utendaji (‘’Executive power’’) inatekelezwa na serikali. Mamlaka ya Uundaji wa sheria vimepewa serikali na Bunge.

Mamlaka ya kuhukumu iko huru kutoka zile ya utendaji na ya uundaji wa sheria.

Serikali ya Malawi imekuwa demokrasia ya vyama vingi tangu mwaka 1994.

Tawi la Mahakama (Executive)

hariri
Main office holders
Idara Jina Chama cha Muda wa Utawala
Rais Arthur Peter Mutharika DPP 14 Mei 2014

Chini ya Katiba ya 1995, rais ambaye pia ni Kiongozi wa Nchi na kiongozi wa Serikali anachaguliwa na raia baada ya kipindi cha miaka mitano. Malawi ina Makamu wa Rais ambaye huchaguliwa na rais mwenyewe. Rais pia ana nafasi ya kumchagua makamu wa rais wa pili, ambaye lazima awe katika chama tofauti. Wanachama wa Baraza la Mawaziri wanaweza kuteuliwa miongoni mwa, au nje ya Bunge. Baraza hili huchaguliwa na rais.

Bakili Muluzi alikuwa rais wa Malawi kuanzia 21 Mei 2004, huku akiwa ameshinda tena baada ya kushinda uchaguzi wa 2000 na asilimia 51.4 ya kura, akimshinda mpinzani wake wa karibu zaidi Gwandaguluwe Chakuamba ambaye alikuwa na asilimia 44.3 kutoka chama cha MCP-AFORD. Mnamo 2004, Bingu wa Mutharika alimshinda tena Chakwamba kwa tofauti ya alama kumi.

Tawi la Bunge

hariri

Bunge la Malawi lina wabunge 193 ambao huchaguliwa na raia wanaowawakilisha kwa kipindi cha miaka mitano. Katiba pia inaruhusu uundaji wa jumba la pili, Senate ambalo huwa na viti 80, lakini hadi leo hakuna harakati zilizotekelezwa kuliunda jumba hilo.

Senate inanuiwa kuunda uwakilishi wa viongozi wa kale na matabaka mbalimbali ya Wilaya, na pia makundi fulani yenye mahitaji ya pekee kama vile wanawake, watoto na walemavu.

Tawi la Mahakama

hariri

Katiba huruhusu Mamlaka ya mahakama ambayo ni huru kutokana na ya Bunge na ya Mamlaka ya Utendaji. Mfumo wa mamlaka ya Mahakama unaiga ule wa Uingereza. Umeundwa na mahakama za Mahakimu (Magisterial) za ngazi za chini, Mahakama Kuu na Mahakama ya Rufaa (Appeal).

Serikali za Mitaa

hariri

Serikali za mitaa zimeundwa na wilaya 28 katika maeneo matatu yanayotawaliwa na Watawala wa Maeneo na Wakuu wa Wilaya ambao wanachaguliwa na serikali kuu. Uchaguzi wa kwanza wa Serikali za mitaa katika historia ya mfumo wa vyama vingi ulifanyika mnamo 21 Novemba 2000. UDF ilishinda asilimia 70 ya viti hivi katika uchaguzi huu.

Wilaya hizo ni:

Ushiriki katika Mashirika ya Kimataifa

hariri

Viungo vya nje

hariri