Sipriani wa Toulon

Sipriani wa Toulon (kwa Kilatini: Cyprianus Tolonensis; Marseille, leo nchini Ufaransa, 4763 Oktoba 546) alikuwa mwanafunzi bora wa Sesari wa Arles, aliyemfanya kwanza shemasi (506), halafu askofu wa Toulon (516)[1].

Sanamu yake.

Katika mitaguso mbalimbali alitetea imani sahihi kuhusu neema dhidi ya Upelajiupande[1], akisisitiza kwamba mtu hawezi kufaidika chochote kutoka mafumbo ya Kimungu, bila kukiomba kwanza kwa neema ya awali ya Mungu[2].

Sesari alipofariki (543), dada yake, Sesaria, alimuomba Sipriani aandike wasifu wake[3], nao ni kati ya vitabu bora vya aina hiyo vya karne ya 6.

Imetufikia pia barua aliyomuandikia askofu Masimo wa Geneva kuhusu masuala mbalimbali ya teolojia [4].

Tangu kale anaheshimiwa na Kanisa Katoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu na babu wa Kanisa.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 3 Oktoba.[5]

Tazama pia

hariri

Tanbihi

hariri
  1. 1.0 1.1 Meier, Gabriel. "St. Cyprian." The Catholic Encyclopedia Vol. 4. New York: Robert Appleton Company, 1908. 30 September 2021
  2. https://www.santiebeati.it/dettaglio/72711
  3. The biography was edited by d'Achery and Mabillon in the Acta Sanctorum Ord. S. Benedicti, Venice 1733, vol. i. p. 636ff, also in the Bollandists' Acta Sanctorum under date of Aug. 27). A modern English translation is W.E. Klingshirn, Caesarius of Arles: Life, Testament, Letters. Translated Texts for Historians, 19 (Liverpool, 1994).
  4. "Saint Cyprian". New Catholic Dictionary. CatholicSaints.Info. 16 September 2012
  5. Martyrologium Romanum

Maandishi

hariri

Vyanzo vingine

hariri
  • Acts of Councils in Gaul, in Concilia Galliae, vol. 2: a. 511-a. 695, ed. by Charles de Clercq, Corpus Christianorum Series Latina, vol. 148a, Turnhout: Brepols 1963 (not translated into English).
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.