Songo Mnara

Coordinates: 9°04′13″S 39°34′58″E / 9.0704°S 39.58288°E / -9.0704; 39.58288


Songo Mnara (pia: Songa Mnara, Songa Manara) ni kisiwa katika funguvisiwa la Kilwa, upande wa kusini mwa Kilwa Kisiwani. Kiutawala ni sehemu ya kata ya Pande Mikoma kwenye Wilaya ya Kilwa, Tanzania.

Kwenye maghofu ya Songo Mnara.

Upande wa mashariki wa kisiwa kuna maghofu ya mji wa kale wa Songo Mnara. Maghofu hayo yamekubaliwa pamoja na yale ya Kilwa Kisiwani katika orodha ya urithi wa dunia wa UNESCO.

Katika karne za 13 - 16 ilikuwa mji muhimu wa biashara ya Bahari Hindi kama inavyojulikana kutokana na mabaki ya bidhaa yaliyopatikana huko[1]. Mabaki ya dhahabu, fedha, lulu, marashi, vyombo vya Uajemi na kauri za China yalipatikana na kuonyesha upana wa biashara ya wenyeji[2].

Wataalamu wa akiolojia walitambua misikiti 6, makaburi 4, nyanja 3 na nyumba zaidi ya 20. Ujenzi ulikuwa wa matumbawe na simiti.[3]

Haijulikani ni nini iliyosababisha kuanguka kwa mji huo lakini kuna dalili za kuwa mwisho wa mji hulingana takriban na wakati wa kufika kwa Wareno katika Afrika ya Mashariki, hivyo kuna watalaamu wanaohisi mvurugo uliosababishwa na kufika kwa Wareno ulileta pia anguko la Songo Mnara.

Tazama piaEdit

PichaEdit

TanbihiEdit

  1. Stoetzel, Jack (2011). "Field Report: Archaeological Survey of Songo Mnara Island". Nyame Akuma 76: 9–14.
  2. Zhao, Bing (March 2012). "Global Trade and Swahili Cosmopolitan Material Culture: Chinese-Style Ceramic Shards from Sane ya Kati and Songo Mnara (Kilwa, ,Tanzania)". Journal of World History 23: 41–85. doi:10.1353/jwh.2012.0018 .
  3. Fleisher, Jeffrey; Wynne-Jones, Stephanie (2012). "Finding Meaning in Ancient Swahili Spatial Practices". African Archaeological Review 29: 171–207. doi:10.1007/s10437-012-9121-0 .

Viungo vya njeEdit

  Kata za Wilaya ya Kilwa - Mkoa wa Lindi - Tanzania  

Chumo | Kandawale | Kibata | Kikole | Kijumbi | Kilwa Masoko | Kipatimu | Kivinje Singino | Kiranjeranje | Lihimalyao | Likawage | Mandawa | Miteja | Mingumbi | Mitole | Namayuni | Miguruwe | Nanjirinji | Njinjo | Pande Mikoma | Somanga | Songosongo | Tingi (Kilwa)


  Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Lindi bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Songo Mnara kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno.