Sophie Oluwole
Sophie Bosede Oluwole (12 Mei 1935 – 23 Desemba 2018), alikuwa mwanafalsafa kutoka nchini Nigeria. Alikuwa mwanamke wa kwanza wa Nigeria aliyepata shahada ya uzamivu au "PhD" katika fani ya falsafa.[1]
Sophie Bosede Oluwole | |
Amezaliwa | 12 mei 1935 [Nigeria ] |
---|---|
Amekufa | 28 desemba 2018 |
Nchi | [Nigeria ] |
Kazi yake | mwanafalsafa |
Maisha na kazi
haririSophie Bosede Oluwole alizaliwa mwaka 1935 katika familia kutoka Edo. Alisoma shule pale Ife. Aliona mfumo wa elimu wa wakati ule ni mgumu kwa wasichana kwa sababu mtazamo wa maisha yao ulikuwa mikononi mwa wazazi, si mwao wenyewe.
Baadaye alisoma historia, jiografia na falsafa kwenye UNILAG (Chuo Kikuu cha Lagos) akaendelea kupata digrii ya kwanza katika falsafa. Mwaka 1972 aliajiriwa kama mhadhiri kwenye UNILAG akaendelea kutimiza masharti ya uzamivu kwenye Chuo Kikuu cha Ibadan. Tangu mwaka 2002 alifundisha tena falsafa ya Kiafrika kwenye UNILAG.
Katika kazi yake alitumia urithi wa kiutamaduni na wa kidini wa Wayoruba. Alisisitiza kuwa urithi huo ulitangulia hata mafundisho ya Sokrates.
Aliaga dunia tarehe 23 Desemba 2018 akiwa na umri wa miaka 83.
Tanbihi
hariri- ↑ "Philosopher urges Nigerians to embrace indigenous knowledge, languages". Retrieved on 2019-10-06. (en-US) Archived from the original on 2019-07-01.
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Sophie Oluwole kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |