Kisangani

Muji mku ya Tshopo ku Jamuuri ya ki Demokratia ya Congo
(Elekezwa kutoka Stanleyville)


Kisangani ni mji mkubwa wa mashariki mwa Kongo wenye wakazi zaidi ya 1,600,000. Ni mji mkubwa wa tatu wa nchi hiyo.

Kisangani
Kisangani is located in Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo
Kisangani
Kisangani

Mahali pa mji wa Kisangani katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo

Majiranukta: 0°31′0″S 25°12′0″E / 0.51667°S 25.20000°E / -0.51667; 25.20000
Nchi Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo
Mkoa Mkoa wa Tshopo
Idadi ya wakazi (2015)
 - Wakazi kwa ujumla 1,602,144
Nembo ya Kisangani.
Kiwanda cha Bralima mjini Kisangani.

Mji uko kando ya mto Kongo mahali ambako mto huu mkubwa umepita maporomoko ya Bayoma na kuwa njia ya maji hadi Kinshasa.

Historia

hariri

Kisangani ilianzishwa na mpelelezi Henry Morton Stanley mwaka 1883 kama kituo cha kampuni ya mfalme Leopold II wa Ubelgiji ikaitwa baadaye Stanleyville hadi mwaka 1966.

Mwanzoni utawala wa Wabelgiji ulikuwa hafifu katika mashariki ya koloni na 1888 mfanyabiashara Mswahili Tippu Tip akafanywa kuwa gavana wa mfalme Leopold II kwa sehemu za mashariki akikaa Stanleyville.

Tangu mwaka 1892 Wabelgiji waliachana na Waswahili wakapigana nao vita na kuchukua utawala mikononi mwao moja kwa moja.

Kisangani iliathiriwa mara nyingi na vita, hasa wakati wa uhuru wa Kongo katika miaka ya 1960 na tangu 1996 katika vita vilivyosababisha anguko la dikteta Mobutu Sese Seko mwaka 1997 na kuendelea katika mapigano kati ya Rwanda, Uganda na vikundi vya Kikongo.

Hivyo hali ya uchumi ni duni ingawa mji una nafasi nzuri kijiografia.

Lugha kuu zinazotumiwa mjini ni hasa Kilingala na Kiswahili.

Tazama pia

hariri

Marejeo

hariri

Viungo vya nje

hariri
 
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  Makala hii kuhusu maeneo ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Kisangani kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.