Open main menu

Kuhusu sisimizi tazama Sungusungu (sisimizi)

Sungusungu ni namna ya kutaja walinzi wa jadi nchini Tanzania. Jina la Sungusungu pamoja asili ya vikundi vyao lilitokea katika jamii za Wasukuma katika Tanzania ya Magharibi.

Jina hili lilianza kupata umaarufu tangu miaka ya 1980 kati ya Wasukuma[1] walioona matatizo ya wizi wa mifugo na ujambazi kwenye barabara baada ya vita ya Uganda na kurudi kwa wanajeshi wengi Tanzania.

Kufuatana nakumbukumbu ya wenyeji, walianzia wilayani Kahama, kata ya Jana na baadaye kuzinduliwa rasmi Kata ya Mwaluguru, mwaka 1982[2]. Baada ya kuona polisi haikuadhibu wezi wa mifugo na kujisikia viongozi kadhaa upande wa serikali walishirikiana nao, wananchi wa Janna waliunda kundi la vijana waliomchagua chifu kati yao na kuwinda wezi. Harakati hii ilienea kwenye kata za jirani. Wezi na majambazi waliuawa mara nyingi lakini vijijini Wasungusungu waliendelea kuwaua pia watu walioshtakiwa kuwa Wachawi. Baada ya polisi kuwatafuta viongozi na kuwakamata Wasungusungu walipata kibali cha rais Julius Nyerere waweze kuendelea[3].

Kati ya Wasukuma kulikuwa na utaratibu wa Wasungusungu; walisimamiwa na "ntemi" wao aliyesaidiwa na makamu wake, "ntwale" na katibu. Chini yao yuko "Kamanda" anayeongoza vijana wanoenda kuwakamata wezi au washtakiwa. Wote walishauriana katika "bunge la Sungusungu".

Kutoka Usukuma mtindo wa sungusungu uliendelea kusambaa kama chombo cha usalama kwa kusaidiwa na vyombo vya dola hadi kuenea juu ya asilimia 20 za Watanzania wote.[4]

Katika miaka ya baadaye mitindo ya ulinzi wa wakazi wa eneo wasio watumishiwa serikali lakini wanashirikiana na vyombo vya serikali imesambaa pia katika miji ya Tanzania[5].

MarejeoEdit

  1. Leticia K. Nkonya, Rural Water Management in Africa: The Impact of Customary Institutions in Tanzania,Cambria Press 2008, ISBN-10: 1604975377, ISBN-13: 978-1604975376, uk. 128, online hapa
  2. Shindikilagi ya Sungusungu ilivyotumika kwa mauaji ‘Operesheni Tokomeza Ujangili’, taarifa ya Shija Felician, kwenye gazeti la Mwananchi, 28/12/2013
  3. Hervé Maupeu & Kimani Njogu, Songs and Politics in Eastern Africa, Mkuki Na Nyota Publishers 2007, ISBN-10: 9987449425, ISBN-13: 978-9987449422, online hapa
  4. Joseph F Donnermeyer, The Routledge International Handbook of Rural Criminology, 2016, uk. 411, ISBN-13: 978-1138799745, ISBN-10: 1138799742 online hapa
  5. https://www.ippmedia.com/sw/safu/tuimarishe-usalama-kwa-maboresho-ya-sungusungu