Ugonjwa wa Parkinson

(Elekezwa kutoka Ugonjwa wa parkinson)

Ugonjwa wa Parkinson (kwa Kiingereza: Parkinson's_disease) ni ugonjwa wa ubongo ambapo mtu hukosa homoni ya dopamini. Hili hutokea baada ya seli zinazotengeneza dopamini kuharibika.

Mchoro wa mwaka 1907 ukionyesha mtu mwenye ugonjwa wa Parkinson.

Dalili ya ugonjwa huu ni kutetemeka kwa mikono (hand tremors), pamoja na shida ya kutembea. Huenda pia mtu akawa na shida za kufikiria. Wagonjwa wa Parkinson huwa na huzuni, utovu wa usingizi pamoja na wasiwasi mwingi.

Ugonjwa huu ulipewa hili jina kwa heshima ya yule anayeaminika kuwa mvumbuzi wake, James Parkinson, aliyeandika mengi kuhusu watu wenye ugonjwa huu katika maandishi aliyoyaita 'An Essay on the Shaking Palsy'.

Kiini cha ugonjwa wa Parkinson

hariri

Haijulikani haswa kiini cha ugonjwa huo lakini yakisiwa kwamba hurithiwa kutoka kizazi kimoja hadi kingine. Sababu za kimazingira huweza pia kuchangia ugonjwa huo; kwa mfano yasemekana kwamba wanaofanya kazi za kupuliza kemikali kwenye mimea huenda wakaupata kwa urahisi. Wanaume huwa kwa hatari kubwa kuupata ugonjwa huu kuliko wanawake.

Matibabu ya ugonjwa wa Parkinson

hariri

Kwa sasa, hamna njia ya kutibu ugonjwa huu lakini kuna dawa ambazo wagonjwa hupewa ili kudhibiti dalili zake. Matibabu hayo ni kama levodopa na sinemet ambayo husaidia kudhibiti mtetemeko, ukosefu wa usingizi, wasiwasi pamoja na dalili nyinginezo za ugonjwa huu. Dawa hizo hufanya kazi kwa muda fulani tu na baadaye huwa hazifanyi. Kifikapo kipindi hicho, wagonjwa hushauriwa kula vizuri na kufanya mazoezi ambayo husaidia pia kudhibiti ugonjwa.

Suala kuhusu matumizi ya bangi iliyoondolewa THC (kiungo kinachomfanya mtu alewe anapovuta bangi) yamekuwa yakijadiliwa ikisemekana kwamba cbd oil husaidia katika kudhibiti kiwango cha dopamini mwilini.

Vifaa maalumu vya wagonjwa wa Parkinson

hariri

Kwa sababu ya kutetemeka, pamoja na shida ya kutembea, wagonjwa wa Parkinson huwa na vifaa maalumu ambavyo wanatumia kuwawezesha kumudu maisha.

Kwa mfano, kuna vijiko vinavyowasaidia kula chakula hata kama wanatetemeka kwa mikono (parkinson spoons). Vijiko hivi huenda vikawa na uzito mwingi kuliko vijiko vya kawaida au viwe na teknolojia ya hali ya juu hivi kwamba vinaweza kujua upande ulioko mdomo na kwa hivyo kudhibiti mtetemeko wa mgonjwa hadi atakapokielekeza chakula kwa mdomo.

Kuna vikombe pia za kusaidia mgonjwa aweze kunywa kinywaji bila ya kumwagika. Vikombe hivyo hutengenezwa kwa muundo utakaoweza kumudu mtetemeko wa mgonjwa wa Parkinson.

Vifaa vingine ni vijiti vya kumsaidia mgonjwa aweze kutembea bila kuanguka kwa kujishikilia wakati wa kutembea[1].

Watu mashuhuri waliokuwa na ugonjwa wa Parkinson

hariri

Tanbihi

hariri
  Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Ugonjwa wa Parkinson kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.