Viktoria wa Abitina

Viktoria wa Abitina alikuwa bikira wa Karthago aliyeuawa pamoja na Wakristo wenzake 48 mwaka 304, wakati wa dhuluma ya kaisari Diokletian, kwa kuadhimisha Siku ya Bwana huko Abitinae[1][2][3], mji wa Afrika Kaskazini (leo Tunisia).

Tarehe 24 Februari mwaka 303, Diokletian alikuwa ametangaza hati yake ya kwanza dhidi ya Wakristo, akiagiza uteketezaji wa Biblia na maabadi ya Kikristo katika Dola la Roma lote, pamoja na kukataza Wakristo wasikutane kwa ajili ya ibada.[4]

Ingawa Fundanus, askofu wa Abitinae, alikubali kukabidhi maandiko matakatifu ya Kanisa kwa serikali, baadhi ya waamini waliendelea kukutana kwa siri chini ya padri Saturninus. Basi, walikamatwa na kupelekwa na mahakimu wa huko hadi Karthago, makao makuu ya mkoa, kwa ajili ya hukumu.[5]

Tarehe 12 Februari gavana Anullinus alisikiliza kesi. Mmoja wa watuhumiwa, Dativus, alikuwa mjumbe wa senati. Ndiye aliyekuwa wa kwanza kuhojiwa, kuteswa na hatimaye kufa.[6][7]

Saturninus alifuata na kushika msimamo katika kuteswa. Wote walifanya vilevile, wanaume kwa wanawake wakiwemo watoto wake 4.

Kati ya majibu waliyotoa hao wafiadini, moja limetajwa mara nyingi: Emeritus, aliyekuwa mwenyeji wa wenzake, alipoulizwa kwa nini aliwakaribishwa kwa ibada kinyume cha sheria, alijibu: "Sine dominico non possumus" ("Hatuwezi kuishi bila ya Bwana").

Tangu kale wafiadini hao wote wanaheshimiwa kama watakatifu.

Sikukuu yao huadhimishwa tarehe 12 Februari. [8]

Orodha ya wafiadini 49 wa Abitina hariri

  • Saturninus wa Abitina, padri
  • Saturninus bin Saturninus
  • Felix bin Saturninus
  • Maria binti Saturninus
  • Hilarion bin Saturninus
  • Dativus, mjumbe wa Senati
  • Felix mwingine
  • Felix mwingine tena
  • Emeritus
  • Ampelius
  • Benignus bin Ampelius
  • Rogatianus
  • Quintus
  • Maximianus au Maximus
  • Telica au Tazelita
  • Rogatianus mwingine
  • Rogatus
  • Ianuarius
  • Cassianus
  • Victorianus
  • Vincentius
  • Caecilianus
  • Restituta
  • Prima
  • Eva
  • Rogatianus mwingine tena
  • Givalius
  • Rogatus
  • Pomponia
  • Secunda
  • Ianuaria
  • Saturnina
  • Martinus
  • Clautus
  • Felix junior
  • Margarits
  • Maior
  • Honorata
  • Regiola
  • Victorinus
  • Pelusius
  • Faustus
  • Dacianus
  • Matrona
  • Caecilia
  • Victoria, bikira kutoka Karthago
  • Berectina
  • Secunda
  • Matrona
  • Ianuaria

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

  1. Jean-Yves Congar, Encyclopedia of Christian Theology (Taylor & Francis 2004 ISBN 978-0-20331901-7). vol. 1, p. 499
  2. Annuario Pontificio 2013 (Libreria Editrice Vaticana 2013 ISBN 978-88-209-9070-1), p. 822
  3. Sancti Aureli Augustini Scripta contra Donatistas, pars I, p. 359
  4. Bleckmann, Bruno. "Diocletianus." In Brill's New Pauly, Volume 4, edited by Hubert Cancik and Helmut Schneider, 429–38. Leiden: Brill, 2002. ISBN 90-04-12259-1
  5. Santi Martiri di Abitina
  6. Dictionary of Christian Biography and Literature to the End of the Sixth Century A.D., with an Account of the Principal Sects and Heresies
  7. Dativo e i martiri di Abitina. Jalada kutoka ya awali juu ya 2008-09-01. Iliwekwa mnamo 2019-09-24.
  8. Under that date the Roman Martyrology records the names of all forty-nine: Martyrologium Romanum (Libreria Editrice Vaticana, 2001 ISBN 88-209-7210-7)

Viungo vya nje hariri