Virginia Centurione Bracelli
Virginia Centurione Bracelli (aliishi Genova nchini Italia 2 Aprili 1587 - 15 Desemba 1651) alikuwa mwanamke tajiri wa mji huo ambaye aliishi muda mfupi katika ndoa halafu akafiwa mumewe akaweka nadhiri ya useja ili kumtumikia Mungu na kuhudumia maskini kwa namna nyingi pamoja na kutegemeza makanisa ya mashambani.
Kwa ajili hiyo alianzisha pia mashirika mawili ya masista[1].
Anaheshimiwa na Kanisa Katoliki kama mtakatifu tangu tarehe 18 Mei 2003, alipotangazwa na Papa Yohane Paulo II; kabla ya hapo Papa huyo alimtangaza mwenye heri tarehe 22 Septemba 1985.
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 15 Desemba kila mwaka[2].
Tazama pia
haririTanbihi
haririViungo vya nje
haririWikimedia Commons ina media kuhusu:
- Daughters of Our Lady on Mount Calvary
- Catholic Forum Archived 20 Februari 2007 at the Wayback Machine.
- Vatican News
- Saints.SQPN: Virginia Centurione Bracelli
- Santiebeati: Virginia Centurione Bracelli
- Catholic Online: Virginia Centurione Bracelli
- Katolsk.no: Virginia Centurione Bracelli
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |