Waklara Wakapuchini
Waklara Wakapuchini ni wanawake wamonaki wanaomfuata Yesu kadiri ya karama ya Fransisko wa Asizi na Klara wa Asizi katika maisha ya sala tu.
Ni kwamba urekebisho wa Ndugu Wadogo Wakapuchini ulisababisha mapema tawi hilo jipya la Waklara linalodumu hadi leo.
Historia
haririMwanzilishi ni Maria Lorenza Llonc (+1542) mjane Mhispania aliyeishi Napoli (Italia) na kuhudumia wagonjwa pamoja na jumuia ya wanawake Wafransisko wasekulari aliyoianzisha. Wakapuchini walipohamia hospitali yake (1529), akawakabidhi uongozi wa jumuia hiyo.
Kati ya 1533 na 1538 wakaongozwa na Mt. Gaetano wa Thiene aliyewaelekeza kwenye maisha ya sala tu na kuwatafutia idhini ya kuishi kimonaki kwa kufuata kanuni ya Mt. Klara (1535). Baadaye akawakabidhi tena Wakapuchini, kwa kuwa karama yao iliathiri sana monasteri hiyo na roho yake, na ndivyo alivyotaka mwanzilishi.
Papa Paulo III (1534-1549) akathibitisha hayo na nia yao ya kushika kikamilifu kanuni (1538). Kwa ajili hiyo mwanzilishi aliikamilisha katiba ya Mt. Koleta Boylet kwa kutumia ile ya Wakapuchini.
Sifa ya monasteri ikaenea haraka na kusababisha kabla ya mwaka 1600 zianzishwe 17 nyingine Italia (Mt. Karolo Boromeo aliunda tatu katika jimbo lake). Ila Wakapuchini wanaume wakakataa katakata kuzisimamia, isipokuwa mbili. Hata hivyo dada zao wakaendelea kuomba msaada huo kwa kuwapitia Maaskofu na wafalme, mpaka Mapapa wakalazimisha hao wanaume kuhudumia walau kiroho monasteri fulanifulani.
Hata nje ya Italia wakaenea haraka: Hispania (1588), Ufaransa (1603), Ureno (1625), Mexico (1665) ambayo ikawa nchi walipoongezeka zaidi hadi leo, Peruu (1713), Gwatemala (1725), Chile (1727) n.k.
Mwishoni mwa mwaka 2005 walikuwa 2,209 katika monasteri 160 duniani.
Viungo vya nje
hariri- Masista katika tovuti ya Ndugu Wadogo Wakapuchini Archived 15 Aprili 2012 at the Wayback Machine.
Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Waklara Wakapuchini kama historia yake, matokeo au athari zake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |