Nicolette Boylet alizaliwa Corbie (Ufaransa) tarehe 13 Januari 1381 katika familia duni.

Sanamu ya Mt. Koleta huko Corbie; ilitengenezwa na Albert Roze (1925).

Ni maarufu kwa kuanzisha urekebisho wa matawi mbalimbali ya Wafransisko ambao walioufuata wanaitwa kwa heshima yake Wakoleta.

Kisha kuishi utawani sehemu mbalimbali, akichukia ulegevu uliotawala huko, alijifungia upwekeni katika nyumba ndogo karibu na kanisa (1402-1406), halafu akajiunga na Wafransisko akakubaliwa na antipapa Benedikto XIII ruhusa ya kurekebisha na kuanzisha monasteri ili zifuate upya ufukara na toba kama walivyofanya na kutaka Fransisko wa Asizi na Klara wa Asizi.

Alifariki tarehe 6 Machi 1447 huko Gand (leo Ubelgiji), katika moja ya monasteri 17 za Waklara alizozianzisha.

Alitangazwa na Papa Klementi XII kuwa mwenye heri tarehe 23 Januari 1740, halafu Papa Pius VII alimtaja kuwa mtakatifu tarehe 24 Mei 1807.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 6 Machi[1].

Tazama pia

hariri

Tanbihi

hariri

Marejeo

hariri

Viungo vya nje

hariri
 
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.