Walter wa Pontoise
Walter wa Pontoise, O.S.B. (pia: Gautier, Gaultier, Gaucher, Gualtierus; Andainville, Picardie, 1030 hivi [1] – Pontoise, Ijumaa Kuu 1099 hivi) alikuwa mmonaki padri wa Utawa wa Mt. Benedikto nchini Ufaransa, ambaye alikubali kuweka pembeni hamu yake ya kuishi upwekeni akaongoza kama abati wa kwanza monasteri karibu na Paris akitoa mfano wake katika kushika kanuni pamoja na kupinga usimoni wa waklero hata akashindana na mfalme Filipo I wa Ufaransa[2].
Mwaka 1094 alianzisha monasteri ya kike.
Alitangazwa mtakatifu na askofu mkuu Hugo wa Rouen mwaka 1153, wa mwisho kutangazwa na mtu asiye Papa katika Kanisa la Magharibi[3][4] “The last case of canonization by a metropolitan is said to have been that of St. Gaultier, or Gaucher, abbat [sic] of Pontoise, by the Archbishop of Rouen, A.D. 1153. A decree of Pope Alexander III, A.D. 1170, gave the prerogative to the pope thenceforth, so far as the Western Church was concerned.”[3].
Tazama pia
haririTanbihi
hariri- ↑ Saint of the Day, May 8: Walter of Pontoise Ilihifadhiwa 8 Aprili 2019 kwenye Wayback Machine. SaintPatrickDC.org. Retrieved 2012-03-05.
- ↑ http://www.santiebeati.it/dettaglio/46690
- ↑ 3.0 3.1 William Smith, Samuel Cheetham, A Dictionary of Christian Antiquities (Murray, 1875), 283.
- ↑ "Biography – Pope Alexander III – The Papal Library". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2013-10-15. Iliwekwa mnamo 2022-10-02.
- ↑ Martyrologium Romanum
Viungo vya nje
hariri- Walter of Pontoise
- Walter of Pontoise Ilihifadhiwa 8 Julai 2011 kwenye Wayback Machine.
- (Kiitalia) San Walter (Gualtiero, Gualterio) di S. Martino di Pontoise
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |