Wasani

(Elekezwa kutoka Wasan)

Wasani (au Wakhoisan) ni kundi la makabila ya Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika ambayo ndio wakazi asili wa maeneo hayo, na ambayo yanachanga sura na lugha kwa kiasi kikubwa, tofauti na Wabantu ambao siku hizi ndio wakazi wake walio wengi.[3]

Mwanamume wa jamii ya Wasani.
Wakushi waliwarithisha Wasani weupe wa ngozi yao[1][2].

Wengi wao walimezwa na makabila hayo, kwa mfano Watswana na Waxhosa.

Nchini Tanzania, waliobaki wa jamii hiyo wanaitwa Wasandawe.

Huko Kusini mwa Afrika wanaishi hasa Namibia, Botswana na Afrika Kusini; baadhi ("San", kwa Kiingereza Bushmen) wamedumisha zaidi taratibu za utamaduni wao kama wawindaji, baadhi ("Khoi", yaani "watu", kwa Kiingereza Hottentots) wameiga ufugaji wa makabila ya Kikushi na ya Kibantu yaliyovamia maeneo yao si zaidi ya miaka 3,000 iliyopita.

Machotara wengi wa leo Kusini mwa Afrika wana asili ya baba Mzungu na mama Khoi.

TanbihiEdit

  1. Pontus Skoglund et al. "Reconstructing Prehistoric African Population Structure", Cell, 2017
  2. Excerpt from The 86th Annual Meeting of the American Association of Physical Anthropologists (2017)
  3. Barnard, Alan (1992) Hunters and Herders of Southern Africa: A Comparative Ethnography of the Khoisan Peoples. New York; Cambridge: Cambridge University Press, 1992.

MarejeoEdit

Viungo vya njeEdit

Wikimedia Commons ina media kuhusu:

TanbihiEdit

  Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Wasani kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.