Wilaya ya Hai

Wilaya ya Hai ni wilaya moja ya Mkoa wa Kilimanjaro. Katika sensa ya mwaka 2002, idadi ya wakazi wa Wilaya ya Hai ilihesabiwa kuwa 210,533.[1]

Mahali pa Hai (kijani) katika mkoa wa Kilimanjaro.

Katika wilaya hiyo wakazi wengi ni Wachaga ambao huzungumza lahaja tofauti, kama Wamachame na Wamasama.

WIlaya hii ilitengwa mwaka 1975 kutoka Wilaya ya Moshi ya awali. Imepakana na Wilaya za Moshi Vijijini (mashariki), Arusha Vijiini na Siha (magharibi). Simanjiro (kusini), Rombo na Mbuga wa Kilimanjaro upande wa kaskazini.

Eneo lake ni kilomita za mraba 1,011. Kiutawala imegawiwa kwa tarafa 3 (Lyamungo, Machame na Masama), kata 14 na vijiji 60. Idadi ya vitongoji ni 248.

Kuna kanda 4 zenye tabianchi tofauti maana wilaya iko kenye mtelemko wa Mlima Kilimanjaro[2]

  • Kanda ya Kilele cha Mlima iko juu ya kimo cha mita 1,800 UB pamoja na kilele cha Kibo. Ni hasa maeneo ya mbuga na hifadhi ya taifa hivyo hakuna wakazi wa kudumu. Ni asilimia 27 za eneo la wilaya.
  • Kanda ya Juu: iko kwenye kimo kati ya mita 1,666 na 1,800 juu ya UB. Inafaa kwa kilimo cha kahawa na ndizi. Walio wengi ni wakulima wadogo wanaofuga pia ng'ombe wa maziwa na kuuza maziwa.
  • Kanda ya Kati: iko kwenye kimo kati ya mita 900 hadi 1,666 juu ya UB. Inapokea mvua kati ya milimita 700 hadi 1250 kwa mwaka; kilimo inafanana na kanda ya juu.
  • Kanda ya Chini iko kwenye kimo chini ya mita 900 juu ya UB. Hapa mvua inapungua hadi milimita 500-700 kwa mwaka. Mazao yanayostawi ni pamoja na maharagwe, mahindi, alizeti na mpunga. Ufugaji hapo chini si hasa ya maziwa ni zaidi ng'ombe wa kienyeji.


MarejeoEdit

  1. Sensa ya 2012, Kilimanjaro - Hai DC[dead link]
  2. Linganisha Investment Profile (taz. viungo vya Nje)

Viungo vya NjeEdit

  • [www.kilimanjaro.go.tz/HAI%20PROFILE%20.doc Hai District Council] - Investment profile
  Kata za Wilaya ya Hai - Mkoa wa Kilimanjaro - Tanzania  

Bomang'ombe | Bondeni | KIA | Machame Kaskazini | Machame Kusini | Machame Magharibi | Machame Mashariki | Machame Narumu | Machame Uroki | Machame Weruweru | Masama Kati | Masama Kusini | Masama Magharibi | Masama Mashariki | Masama Rundugai | Mnadani | Muungano | Romu


  Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Kilimanjaro bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Wilaya ya Hai kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.


Isipokuwa usitaje majina ya viongozi waliopo sasa maana wanabadilika haraka mno.