William Tate Olenasha

William Tate Olenasha (27 Mei 1972 - 27 Septemba 2021) alikuwa mwanasiasa Mtanzania na mwanachama wa chama cha kisiasa cha CCM. Alichaguliwa kuwa mbunge wa Ngorongoro kwenye chaguzi kuu za mwaka miaka 2015 na 2020. [1] Mwaka 2020 alifanywa kuwa Naibu Waziri Uwekezaji katika ofisi ya Waziri Mkuu.

Alifariki dunia 27 Septemba 2021 jijini Dodoma baada ya kuwa mgonjwa kwa siku chache[2].

Olenasha alizaliwa katika familia ya Kimaasai akasoma shule ya msingi huko Kakesio, Wilaya ya Ngorongoro (1978 - 1984) akaongeza elimu ya sekondari kwenye shule ya seminari katoliki Arusha (1986-1992). Kwenye Chuo Kikuu cha Dar es Salaam alihitimu shahada ya awali ya sheria mwaka 1999 na digrii ya uzamili kwenye Chuo Kikuu cha Pretoria mnamo 2001.

Miaka 2002-2005 alifanya kazi kenye PINGO's Forum, ambayo ni shirika la kutetea maslahi ya wafugaji asilia kimataifa.

Miaka 2005 hadi 2009 alihamia Oxfam alipokuwa bingwa wa changamoto za wafugaji. Hadi mwaka 2015 aliendelea kuwa mshauri wa serikali ya Sudan Kusini na kushiriki katika makampuni ya wanasheria wa Tanzania.

Mwaka 2015 alijiunga na siasa akawa mbunge na naibu waziri wa kilimo, ufugaji na uvuvi.

Marejeo hariri

  1. Tovuti ya Bunge la Tanzania, iliangaliwa Mei 2017
  2. Tanzania’s Investment Deputy Minister Ole Nasha dies at 49 Archived 28 Septemba 2021 at the Wayback Machine., gazeti la Citizen tar. 28.09.2021