Willian Borges da Silva (kwa kawaida anajulikana kama Willian; alizaliwa Agosti, 1988, ni mchezaji wa Brazil, ambaye anacheza kama kiungo mshambuliaji katika klabu ya Corinthians na timu ya taifa ya Brazil.

Willian (2015)

Maisha

hariri

Willian alianza kucheza katika timu ya Brazil mwaka 2011 na aliliwakilisha taifa lake katika Kombe la Dunia la FIFA ya 2014, Copa America ya 2015 na Copa America Centenario.

Anzhi Makhachkala

hariri

Mnamo tarehe 31 Januari 2013, Willian alihamia Anzhi Makhachkala. Awali alichagua kuvaa namba 10, hata hivyo kutokana na vikwazo vya UEFA ambavyo inasema mchezaji lazima avae nambari inayotumiwa katika Ligi ya Mabingwa, alilazimika kuvaa namba 88 aliyoichagua akiwa Shakhtar.

Baada ya kuhamia Urusi, Willian alisema alifurahi kujiunga na Anzhi na aliitakia Shakhtar Donetsk mafanikio makubwa katika siku zijazo. Kwa mara ya kwanza, Willian alishambulia Newcastle United katika Ligi ya Europa.Pia alifunga bao lake la Anzhi pekee mnamo 14 Aprili 2013 katika ushindi wa 3-0 dhidi ya Volga Nizhny Novgorod.

Chelsea

hariri
 
Willian akichezea klabu ya Chelsea

Mnamo tarehe 25 Agosti 2013, klabu ya Uingereza ya Ligi Kuu ya Chelsea ilikubali kusainiwa kwa Willian. Mpango huo ulifanyika rasmi tarehe 28 Agosti 2013 na Willian alijiunga kwa mkataba wa miaka mitano, akipokea shati namba 22 mgongoni.

Willian alianza kucheza rasmi katika klabu ya Chelsea mnamo tarehe 18 Septemba dhidi ya Basel katika Ligi ya Mabingwa. Baada ya kushinda dhidi ya Swindon Town na Steaua Bucureşti katika Kombe la Ligi ya Mabingwa,Chelsea ilicheza mechi dhidi ya Norwich City mnamo terehe 6 Oktoba na kushinda 3-1.Pia aliisaidia Chelsea kushinda 2-0 dhidi ya Liverpool.

  Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Willian kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.