Yoana Beretta Molla

Gianna Beretta Molla (Magenta, Lombardia, Italia, 4 Oktoba 1922Monza, 28 Aprili 1962) alikuwa daktari bingwa wa maradhi ya watoto.

Picha yake halisi.

Mke wa Pietro Molla, alipokuwa mjamzito kwa mara ya nne, alipatikana na ugonjwa ambao tiba yake ilitaka mimba yake ife asije akafa mwenyewe. Ingawa alijua vizuri hilo, alikataa tiba kamili ili mtoto aweze kuzaliwa.

Papa Yohane Paulo II alimtangaza mwenye heri tarehe 24 Aprili 1994 na mtakatifu tarehe 16 Mei 2004 mbele ya mume na watoto wake wote.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe ya kifo chake[1].

Tazama pia

hariri

Maandishi yake

hariri
  • Molla, Gianna Beretta, Love Letters to My Husband, Guerriero, Elio, ed., Pauline Books, 2002.

Tanbihi

hariri
  1. Martyrologium Romanum: ex Decreto Sacrosancti oecumenici Concilii Vaticani II instauratum auctoritate Ioannis Pauli P.P. II promulgatum, Romae 2001, ISBN 8820972107

Viungo vya nje

hariri
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.