Alberto wa Pontida

Alberto wa Pontida, O.S.B. (Prezzate, 1025; † 2 Septemba 1095), alikuwa abati huko Lombardia, Italia.

Mtakatifu Alberto wa Pontida.

Alberto alikuwa kati ya wamonaki waliojitahidi zaidi kueneza urekebisho wa Cluny katika mkoa huo. Hata hivyo, alikuwa upande wa kaisari Henri IV wa Ujerumani katika mashindano yake na Papa Gregori VII.

Anaheshimiwa na Kanisa Katoliki kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 2 Septemba pamoja na mtakatifu Vitus[1].

Maisha hariri

Kabla hajajiunga na umonaki, alikuwa askari kufuatana na kawaida ya koo maarufu za wakati huo. Ni baada ya kujeruhiwa sana vitani kwamba aliamua kufuata maisha ya Kiroho.

Alipokwenda kuhiji Santiago de Compostela (Hispania) alipitia monasteri kadhaa za Waklunii na kuvutiwa sana na maisha ya namna hiyo.

Aliporudi nyumbani alijitolea mali yake kuanzisha monasteri (1059).

Baadaye alikwenda kupata malezi ya Ugo wa Cluny kwa miaka saba.

Tena akarudi Pontida kuongoza monasteri yake na kuanzisha nyingine kwa wanawake.

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

  1. Martyrologium Romanum

Marejeo hariri

  • G.M. Cantarella, I monaci di Cluny, Einaudi, Torino, 1997;
  • J. Huizinga, L'autunno del Medioevo, Newton-Compton, Roma, 1997;
  • J. Le Goff, L'uomo medievale, Laterza, Bari, 1999;
  • Cognomi e famiglie del bergamasco, S.E.S.A.A.B., Bergamo, 2000
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.