Alferi, O.S.B. (kwa Kiitalia: Alferio; Salerno, 930 - Cava de' Tirreni, Salerno, 12 Aprili 1050) aliacha mwaka 1002 maisha ya ikulu akawa mmonaki huko Cluny nchini Ufaransa chini ya Odilo.

Mt. Alferi akipata njozi ya Utatu Mtakatifu.

Baada ya kupata upadirisho huko aliitwa na mtemi wa Salerno akarekebishe monasteri nyingi za huko. Kumbe, baada ya muda alijitenga upwekeni pamoja na wenzake wawili na mwaka 1011 hivi kuanzisha ile maarufu ya Cava akawa abati wake wa kwanza hadi alipofariki dunia akiwa na umri wa miaka 120[1].

Tangu kale anaheshimiwa na Kanisa Katoliki kama mtakatifu. Heshima hiyo ilithibitishwa na Papa Leo XIII tarehe 21 Desemba 1893.

Sikukuu yake inaadhimishwa kila tarehe 12 Aprili[2].

Tazama pia

hariri

Tanbihi

hariri

Marejeo

hariri
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.