Ana Schaeffer (Mindelstetten, Bavaria, Ujerumani, 18 Februari 1882 – Mindelstetten, 5 Oktoba 1925), alikuwa mwanamke mwenye karama za pekee katika maisha ya ugonjwa[1] nyumbani akizama katika sala.

Picha halisi ya Mt. Ana.

Ni kwamba, alipokuwa na umri wa miaka 19, akiwa mfanyakazi wa ndani, alimwagikiwa maji ya moto, tukio lililozidi kuathiri vibaya afya yake; hata hivyo aliishi kwa utulivu katika ufukara, akimtolea Mungu msalaba wa maumivu yake kwa ajili ya wokovu wa watu[2].

Mwaka 1910 alijikuta ana madonda mwilini kama yale ya Yesu msulubiwa[3]. Pia alipata njozi[4].

Alitangazwa na Papa Yohane Paulo II kuwa mwenye heri tarehe 7 Machi 1999[5], halafu Papa Benedikto XVI alimtangaza mtakatifu tarehe 21 Oktoba 2012[6].

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 5 Oktoba[7].

Tazama pia

hariri

Tanbihi

hariri
  1. "Kościół ma siedmioro nowych świętych" Deon.pl, October 21, 2012
  2. https://www.santiebeati.it/dettaglio/92086
  3. Rommel C. Lontayao. "Blessed Anna Schaffer: A life of pain and suffering". Manila Times, January 22, 2012.
  4. Radio Vaticana. "The canonization of Anna Schäffer: Interview with postulator". October 20, 2012.
  5. During her beatification, 7 March 1999, Pope John Paul II said: "If we look to Blessed Anna Schäffer, we read in her life a living commentary on what Saint Paul wrote to the Romans: 'Hope does not disappoint, because the love of God has been poured out into our hearts through the Holy Spirit that has been given to us' (Rom. 5:5). She most certainly was not spared the struggle to abandon herself to the will of God. But she was given to grow in the correct understanding that weakness and suffering are the pages on which God writes His Gospel ... Her sickbed became the cradle of an apostolate that extended to the whole world."
  6. Breslin, Carole (3 Oktoba 2017). "Catholic Heroes... St. Anna Schaffer". TheWandererPress.com. Iliwekwa mnamo 11 Januari 2019.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  7. Martyrologium Romanum

Viungo vya nje

hariri
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.