Angata Barrikoi ni kata inayopatikana katika kaunti ya Narok, Kenya.

Mtaa mdogo wa Angata Barrikoi.

Eneo ni la km² 315.20.

Watu hariri

Ina watu wanaokadiriwa 24,945 (2019) na vijiji vidogo kama: Kabusa, Oldonyorok, Ongata, Tebengwet, Kabchinese, Kabwolta, Kondamet, Leoboinet na Sacfo.

Makabila hariri

Kuna makabila mengi kama Wakikuyu, Wakisii lakini Wakipsigis ni 10,000. Kuna Wasomali ambao wanafanya biashara katika maduka.

Dini hariri

Kuhusu dini, wanakadiriwa watu elfu kumi ni Wakristo, lakini watu wengi huchanganya dini za jadi na za Kikristo, hivyo ni ngumu kutambua. Wengi ni Waprotestanti na mia tisa ni wa dini za jadi.

Hakuna msikiti.

Kilimo na ufugaji hariri

Watu wengi wanafuata ufugaji wa ng'ombe na pia mbuzi na kondoo. Lakini pia watu wanalima hasa mahindi na pia maharagwe. Mboga kama sukuma wiki pia inapendwa sana na kuliwa na watu wengi.

Masoko hariri

Kuna vijisoko vidogo kama: soko la Ongata na la Oldonyorok. Pia kuna maduka mengi na maghala ambapo nafaka kama mahindi huwekwa na kuuzwa. Pesa zinazotumika ni Shilingi ya Kenya na Shilingi ya Tanzania.

Masomo hariri

Shule nyingi zimejengwa ili wanafunzi wasome[1], kama shule za sekondari za Ongata[2] na 0ldonyorok. Pia kuna vyuo vingi, hasa cha Oldonyorok, ambapo mambo ya ufundi hufundishwa.

 
Basi la shule ya Angata Barrikoi.

Afya hariri

Vituo vya matibabu ni vichache mno, kituo kinachojulikana ni Angata Health Centre[3][4]. Kuna famasia nyingi hasa katika maduka ya Angata na Oldonyorok.

Michezo hariri

Kuna timu ya mpira wa miguu inayoitwa Angata Victors FC.

Tanbihi hariri

Viungo vya nje hariri