Aurelia wa Aleksandria

Aurelia wa Aleksandria (243 hivi - 2 Desemba 260) alikuwa msichana wa mji huo wa Misri, ambaye pamoja na mama yake Martana alihamia Roma walipokuwa wamefia dini binamu zake Adria na Paulina pamoja na watoto wao Neone na Maria.

Miezi michache baada ya kuolewa huko, na kumfanya mume wake abatizwe, aliuawa kwa kukataa kutoa ubani kwa miungu. Jana yake aliona mama yake na dada ya mama wakikatwa kichwa kwa sababu hiyohiyo, naye mahali pale akafanyiwa vilevile.

Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu mfiadini.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe ya kifo chake[1].

Tazama pia

hariri

Tanbihi

hariri
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.