Upara

(Elekezwa kutoka Baldness)

Upara (kwa Kiingereza baldness) ni hali ya kutokuwa na nywele au ukosefu wa nywele mahali ambapo mara nyingi hukua, hasa kichwani. Aina ya upara ya kawaida zaidi ni upungufu wa nywele unaowatokea hatua kwa hatua binadamu wanaume na viumbehai wengine na ambayo huitwa "mkondo wa upara wa kiume".

Alopecia
Mwainisho na taarifa za nje
Kundi MaalumuInfectious diseases Edit this on Wikidata
ICD-10L65.9
ICD-9704.0
DiseasesDB14765
MeSHD000505

Kiasi na mikondo ya upara vinaweza kutofautiana sana, baina ya mikondo ya kiume na ya kike ya alopeshia (androgenic alopecia au alopecia androgenetica), alopecia areata, ambayo huhusisha upotevu wa baadhi ya nywele kichwani na alopecia totalis, ambayo huhusisha upotevu wa nywele zote kichwani, hadi aina iliyokithiri zaidi ambayo ni universalis alopecia, inayohusisha kupoteza nywele zote kichwani na mwilini.

Asili ya jina la kimataifa

hariri

Istilahi alopeshia hutokana na neno la Kigiriki αλώπηξ, alópex, inayomaanisha mbweha. Asili ya matumizi hayo ni kuwa mnyama huyu huvua manyoya yake mara mbili kwa mwaka.

Dalili

hariri

Ishara ya upara ni ukosefu wa nywele juu ya kichwa cha mtu.

Sababu

hariri

Matukio ya upara wa kiolezo hutofautiana miongoni mwa idadi kubwa ya watu kwa misingi ya maumbile ya jeni; sababu za kimazingira hazionekani kuathiri sana aina hii ya upara. Utafiti mmoja mkubwa uliofanywa katika Maryborough, Victoria, Australia ulionyesha kuwa kiwango cha ya upotezaji nywele za mbeleni mwa kichwa-katikati hulingana na ongezeko la umri na huathiri 73.5% ya wanaume na 57% ya wanawake wenye umri wa miaka 80 na zaidi. Kwa mujibu wa tovuti ya Medem Medical Library, upara wa kiume huathiri takribani wanaume milioni 4 nchini Marekani. Takriban asilimia 25 ya wanaume huanza kupata upara tokea umri wa miaka 20, theluthi mbili huanza kupata upara kuanzia miaka 60. Uwezekano wa kupata jeni ya upara ni 4 kwa 7.

Mkondo wa wanaume hudhihirisha upungufu wa nywele kutoka pande za paji la kichwa unaojulikana kama "upeo wa nywele unaopungua". Upungufu wa upeo wa nywele huonekana katika wanaume waliozidi miaka 20 lakini unaweza kuonekana mapema, mwishoni mwa umri wa ujana pia.

Sehemu ndogo ya upara inaweza kujitokeza sehemu ya juu (vertex). Sababu za aina hii ya upara (uitwao androjenetic alopecia) ni DHT, homoni yenye msukumo wa nguvu za ngono, ukuaji wa nywele za mwilini na usoni, ambayo huweza kuathiri vibaya tezi kibofu pamoja na nywele za kichwani.[1]

Bado haijafahamika kikamilifu namna ambayo DHT hutekeleza jambo hili. Kwenye ngozi za vichwa zinazoathirika na jeni hii, DHT huzua mchakato wa ukondefu wa nywele. Kupitia mchakato wa ukondefu wa nywele, upana wa mzizi wa nywele huendelea kupungua kitaratibu hadi nywele kwenye ngozi ya kichwa kufanana na manyoya hafifu au "sufi za pichi" au hata kutoweka kabisa. Mwanzo wa kupoteza nywele wakati mwingine huanza mapema mwishoni mwa ubalehe na hasa husababishwa na jeni. Upara wa mkondo wa kiume huainishwa katika kipimo cha Hamilton Norwood I-VII.

Iliaminika awali kuwa upara ulirithiwa kutoka kwa babu wa ukoo wa mama. Ingawa pana misingi ya imani hii, wazazi wote huchangia uwezekano wa vizalia wao kupoteza nywele. Pana uwezekano mkubwa zaidi wa kurithi upara iwapo mchanganyiko wa jeni zinazosheheni kwa nguvu kutoka wazazi wote zina hali hiyo.

Kuna aina nyingine nyingi za upara:

  • Alopeshia ya mvuto hupatikana kwa kawaida kwa watu wenye nywele ndefu zifungwazo kwa nyuma au mistari ambao huvuta nywele zao kwa nguvu nyingi.
  • Trikotilomania ni upoteaji wa nywele unaosababishwa na uvutaji au ukunjaji shurutishi wa nywele. Hutokea zaidi kwa watoto kuliko watu wazima. Katika hali hii, nywele hazitoweki kichwani, bali hukatika. Nywele zinapokatika karibu na ngozi ya kichwa husababisha nywele fupi zenye umbo la "alama ya mshangao."
  • Kiwewe kama vile cha kemotherapia, kujifungua, upasuaji mkubwa, sumu na mfadhaiko kali kinaweza kusababisha upotevu wa nywele unaojulikana kama effluviamu ya telojeni.[2] Mzizi wa nywele katika awamu ya kukua huathirika na kemotherapia wakati matibabu hayo hulenga kutenganisha seli za saratani. Kwa hiyo, karibu asilimia 90 ya nywele hudondoka punde tu baada ya kemotherapia kuanza.[3]
  • Kupoteza nywele kunakotia shaka aghalabu hufuatia kujifungua pasipo kusababisha athari upara halisi. Katika hali hii, nywele kwa hakika hunawiri wakati wa mimba kutokana na ongezeko la estrojeni mwilini. Baada ya mtoto kuzaliwa, viwango vya estrojeni hushuka hadi viwango vya kawaida vya kabla-ya-mimba, nayo mizizi ya ziada ya nywele hudondoka. Hali kama hiyo hutokea kwa wanawake wanaotumia dawa ya kuchochea ushikaji-mimba ya clomiphene.
  • Upungufu wa chuma ni sababu ya kawaida ya ukondefu wa nywele, ingawa upara halisi si kawaida kuonekana.
  • Mnururisho unaoangazwa ngozini mwa kichwa, kama wakati wa rediotherapia, hutumika kwa minajili ya kutibu baadhi ya saratani humo, nao huweza kusababisha upara katika maeneo yaliyoathirika.
  • Baadhi ya maambukizi ya maikoti yanaweza kusababisha upotevu mkubwa wa nywele.[4]
  • Alopeshia areata ni mvurugiko wa mfumo wa kingamwili ambao pia hujulikana kama "upara wa doa" na ambao unaweza kusababisha kupotea kwa nywele kuanzia eneo moja tu (Alopecia areata monolocularis) hadi katika mwili mzima (Alopecia areata univesalis).
  • Upotevu wa nywele wa eneo moja au uliotawanyika huweza pia kutokea katika alopeshia sikatrishia (lupus erithematosu, licheni plano pilari, folliculitis dekalvansi, sentrifugi sikatrishia alopeshia ya kati, alopeshia fibrosi ya mbele baada ya kukoma uzazi, nk). Uvimbe na michipuko ngozini pia husababisha upara wa eneo moja (neva ya sebashia, seli ya msingi ya kasinoma, seli ya juu ya karsinoma).
  • Hipothairoidi inaweza kusababisha kupotea kwa nywele za mbele kwa kawaida, na huhushwa hasa na ukondefu wa thuluthi ya nje ya kope za macho (kaswende pia inaweza kusababisha upotevu wa thuluthi ya nje ya kope za macho)
  • Hipathairoidi pia inaweza kusababisha kupotea kwa nywele, ambayo kwa njia sawa na siyo tu mbele.
  • Kupoteza nywele kwa muda kunaweza kutokea katika maeneo ambapo uvimbe wa ngozi umekuwepo kwa muda; kwa kawaida tokea muda wa wiki moja hadi wiki kadhaa.
  • Alopeshia ya pembetatu ya muda mrefu - Upotevu wa nywele ulio na umbo la pembetatu au duaradufu kwa baadhi ya nyakati, katika eneo la kandokando ya kichwa ambayo hutokea hasa kwa watoto wadogo. Eneo lililoathirika hasa huwa na mizizi kondefu ya nywele au mizizi hiyo hutoweka kabisa, lakini halipanuki. Sababu zake hazijulikani na ingawa ni hali ya kudumu, haina madhara mengine yoyote kwa walioathirika.[5]

Nadharia tete za mageuko ya kimaumbile

hariri

Hakuna makubaliano kuhusu maelezo ya mageuzi ya mkondo wa upara wa kiume. Madai ya kwamba mkondo wa upara wa kiume (MPB) hunuiwa kuwasilisha ujumbe wa kijamii unaungwa mkono na ukweli kwamba msambao wa vihisivu androjeni kwenye ngozi ya kichwani hutofautiana baina ya wanaume na wanawake, aidha waume na wake wazee walio na viwango vya juu vya androjeni mara nyingi hudhihirisha ukondefu wa nywele uliotawanyika, kinyume na ilivyo katika mkondo wa upara wa kiume.

Nadharia moja, iliyotolewa na Muscarella na Cunningham,[6] inaeleza kuwa upara ulijitokeza miongoni mwa wanaume kufuatia uteuzi wa jinsia kama ishara pevu ya uzee na ukomavu wa kijamii, ambapo uchokozi na tabia za kujihatarisha huongezeka. Hii ilitoa taswira ya mwanamume aliyefikia hali iliyoimarika kijamii lakini aliyepungukiwa na uwezo wa kimwili wa kupata washirika wa kujamiiana na kukuza watoto hadi utu uzima.

Katika utafiti wa Muscarella na Cunningham[6] , wanaume na wanawake walitazama wanamitindo 6 wa kiume waliokuwa na viwango tofauti vya nywele usoni (walio na ndevu na masharubu au bila) na nywele kichwani (kichwa kilichojaa nywele, zinazopungua na upara). Washiriki walitathmini kila mafungu kwa kutumia vivumishi 32 vilivyohusiana na mitazamo ya jamii. Wanaume waliokuwa na upara ama waliokuwa na nywele usoni au nywele zinazopungua walichukuliwa kuwa wenye umri mkubwa zaidi kuliko wale ambao waliokuwa wamenyolewa kabisa au waliokuwa na nywele nyingi kichwani. Ndevu na kichwa kilochojaa nywele zilionekana kama hali ya ujasiri zaidi na kutokomaa kijamii, nao upara ukahusishwa na ukomavu zaidi kijamii. Hariri ya maoni ya kijamii kuhusu mikondo ya upara wa kiume umetolewa na Henss (2001).[7]

Nadharia tete nyingine za mageuko ya kimaumbile ni pamoja na miunganiko baina ya jeni kwa sifa bainishi zenye manufaa zisizohusiana na nywele wala utofauti wa jeni.

Upara usio wa binadamu

hariri

Upara si tu ni sifa bainishi ya binadamu. Viumbe wengine wa jamii ya nyani, kama vile masokwe, makakiu wenye mikia minene, na uakari wa Amerika ya Kusini hudhihirisha ukondefu taratibu wa nywele kichwani baada ya kubalehe. Makakiu wazima wenye mikia minene, kwa kweli, hutumika mara nyingi maabarani katika kutafiti matibabu yasaidiayo ukuaji wa nywele.

Watangulizi mbalimbali wa tai wa Ulimwengu wa Kale na Ulimwengu Mpya waligeuka kwa kipindi cha wakati na kupata upara kichwani, iliyozuia manyoya kushika vipande vya nyama zilizooza kutoka mlo wa tai, na kusaidia pia kupunguza joto.[8]

Jenetikia

hariri

Utafiti mwingi ulifanywa kuhusu maumbile ya jeni zinazohusiana na mkondo wa upara wa kiume, au androgenetic alopecia (AGA). Utafiti unaonyesha kwamba kwa kiasi kikubwa, uwezekano wa kupatwa na upara wa mapema wa kiume hutokana na jeni za chembeuzi X. Jeni nyingine zisizohusiana na ngono pia hushirikishwa.

Watafiti wa Ujerumani wanataja jeni pokezi ya androjeni kama kiungo muhimu zaidi cha upara.[9] Wanahitimisha kwamba aina fulani ya jeni pokezi ya androjeni huhitajika kwa ukuaji wa AGA. Mwaka huohuo matokeo ya utafiti huu yalithibitishwa na watafiti wengine.[10] Jeni hii ni dhaifu, kwa hivyo mwanamke huhitaji kromosomu mbili za X zenye kasoro ili kuonyesha alopeshia ya mkondo sawa na wa kiume. Kwa vile androjeni na mahusiano yake na kipokezi cha androjeni ndiyo sababu za AGA inaonekana jambo la kimantiki kuchukulia kuwa jeni hisivu ya androjeni ina jukumu muhimu katika ukuaji wake.

Utafiti mwingine wa mwaka 2007 ulipendekeza kuwa jeni nyingine katika kromosomu X, iliyo karibu na jeni pokezi ya androjeni, ilikuwa na jukumu muhimu katika mkondo wa upara wa kiume. Walipata kuwa eneo la Xq11-q 12 katika kromosomu X- lilihusiana pakubwa na AGA katika wanaume. Walisisitiza kuwa EDA2R ndiyo jeni inyohusiana zaidi na AGA. Utafiti huu umeigwa katika angalau tafiti tatu huru zifuatazo.

Jeni nyinginezo zinazohusika na upotevu wa nywele zimegunduliwa. Mojawapo ikiwa jeni ya kromosomu 3. Jeni huwa iko katika 3q26.[11] Jeni hii pia huchangia katika aina ya upara unaohusishwa na ulemavu wa akili. Jeni hii ni dhaifu.

Jeni nyingine ambayo inaweza kushiriki katika upotevu wa nywele ni P2RY5. Jeni hii inahusika na muundo wa nywele. Baadhi zinaweza kusababisha upara wakati wa kuzaliwa ilhali aina nyinginezo husababisha "nywele za sufu".[12]

Utafiti wa hivi karibuni ulithibitisha jeni pokezi X zinazohusiana na androjeni kuwa za muhimu zaidi. Huku jeni katika kromosomu 20 ikiwa ya pili kwa umuhimu wa kuchangia hali hiyo (snpedia)

Upotezaji nywele kwa wanawake

hariri

Ingawa upara si kawaida sana katika wanawake kama ilivyo kwa wanaume, athari za kisaikolojia za kupoteza nywele huwa kubwa zaidi. Kwa kawaida ukanda wa nywele za mbele hudumu ilhali uwingi wa nywele hupungua katika maeneo yote kichwani. Hapo awali iliaminika kuwa ilisababishwa na testosteroni sawa na katika upara wa kiume, lakini wanawake wengi ambao kupoteza nywele huwa na viwango vya kawaida vya testosteroni.

Hata hivyo, upotezaji nywele kwa mwanamke umekuwa tatizo linaloendelea, ambalo kwa mujibu wa Akademia ya Marekani ya Matibabu ya ngozi, huathiri karibu wanawake 30,000,000nchini Marekani. Ingawa upotezaji nywele kwa wanawake kwa kawaida hutokea baada ya umri wa miaka 50 au hata baadaye, isipoambatana na matukio kama ujauzito, maradhi sugu, ya mlo, na mfadhaiko kati ya nyinginezo, kwa sasa inatokea miaka ya mapema na huku ripoti zikionyesha kuwa hutokea hata wanawake wachanga kama wa miaka 15 au 16.[13]

Sababu za upotevu wa nywele mingoni mwa wanawake zinaweza kutofautiana na zinazoathiri wanaume. Kuhusiana na alopeshia androjeni, upotevu wa nywele za wanawake hutokea kulingana na athari za homoni za androjeni (testosteroni, androsteinedioni, na dihaidrotestosteroni (DHT)). Homoni hizi za kiume, kwa kawaida hutokea kwa kiasi kidogo kwa wanawake.

Hata hivyo, kulingana na Ted Daly, MD, tabibu wa ngozi kutoka Kituo cha Matibabu cha Chuo Kikuu cha Long Island, alopeshia androjeni sio sababu kuu ya kupotea kwa nywele kwa wanawake na wataalamu wa ngozi kwa sasa hupendelea kuita hali hii mkondo wa upotevu wa nywele kwa wanawake badala ya kutumia neno androjeni alopeshia. Anaongeza kuwa mkondo wa kike ni wa mtawanyiko na hudhihirika katika eneo lote la juu ya kichwa na waweza kuathiri wanawake wakati wowote.[14]

Wakati mwingine pia mchakato wa homoni huweza kusababisha upotevu wa nywele kwa mwanamke. Baadhi ya mifano ni: uja uzito, kufikia kutoweza kuzaa, uwepo wa uvimbe wa ovari, dawa za kudhibiti upataji mimba na kiwango juu cha androjeni, dalili za vimbe nyingi za ovari. Pia matatizo ya tezi, anemia, ugonjwa sugu na baadhi ya dawa husababisha upotevu wa nywele kwa mwanamke .[15]

Utunzaji

hariri

Athari za kisaikolojia

hariri

Alopeshia kutokana na kemotherapi ya saratani imeripotiwa kusababisha mabadiliko katika dhana-nafsia na taswira ya mwili. Taswira ya mwili hairejelei hali ya awali baada ya kuota upya kwa nywele kwa idadi kubwa ya wagonjwa. Katika hali kama hizo, wagonjwa hutatizika kuonyesha hisia zao (alexithymia) na hutaka zaidi kujiepusha na migogoro ya familia. Tiba ya familia inaweza kusaidia familia kukabiliana na matatizo ya kisaikolojia yakijitokeza.[16]

Matatizo ya kisaikolojia kutokana na upara, yakiwepo, kwa kawaida hushamiri zaidi mwanzoni mwa dalili.[17]

Baadhi ya wanaume wenye upara huonea fahari upara wao, wakihisi unasaba na watu maarufu wenye haiba walio na upara kama vile Yul Brynner, Bruce Willis, Vin Diesel, Sean Connery, Jason Statham, Patrick Stewart, Ben Kingsley, "Stone Cold Steve Austin, Tupac Shakur, Michael Chiklis , Telly Savalas, na Jeffrey Eugenides. Larry David hasa hutumia upara wake kama njia ya ucheshi-nafsia katika vipindi vyake vya televisheni vya Seinfeld and Curb Your Enthusiasm. Katika miaka ya hivi karibuni, upara ,umekuwa si tatizo kubwa kutokana na ongezeko la mtindo wa kudumisha nywele fupi sana, au hata kunyoa nywele kabisa, miongoni mwa wanaume katika nchi za magharibi. Kwa mfano, Patrick Stewart alitajwa kama "Mume wa Kuvutia zaidi kwenye TV" kwa jukumu lake la haiba kama Kapteni Jean-Luc Picard.

Makampuni mengi yamefanikiwa kibiashara kwa kuuza bidhaa ambazo hugeuza hali ya upara, kwa ukuzaji nywele upya, upandikizaji nywele kwa upasuaji au kuuza vibandiko vya nywele.

Kuzuia na kugeuza upotevu wa nywele

hariri

Matibabu ya aina mbalimbali za alopeshia huwa na mafanikio madogo. Baadhi ya waliopoteza nywele hutumia matibabu yaliyothibitika kiafya kama vile finasteridi, dutasteridi na mchanganyiko wa minoksidili inayotumiwa katika jaribio la kuzuia upotevu zaidi ya nywele na kuikuza upya. Kama kanuni ya jumla, ni rahisi kudumisha nywele zilizosalia kuliko kukuza upya, hata hivyo, matibabu yaliyotajwa yanaweza kuzuia kupotea kwa nywele kutokana na Androjeni alopeshia , na kuna teknolojia mpya katika upasuaji wa kujirembesha wa kupandikiza na mifumo ya uwekaji nywele ambayo huenda yasitambulike kabisa.

Nchini Marekani pana tiba aina mbili za dawa, ambazo zimeidhinishwa naShirika la Usimamizi wa Chakula na Dawa la Marekani (FDA) ikiwemo bidhaa moja iliyokubaliwa na FDA kwa matibabu ya alopeshia androgeni, inayojulikana pia kama mkondo wa kupoteza nywele wa kiume au wa kike. Matibabu mawili yaliyoidhinishwa na FDA ni finasteridi (inayotangazwa kama propeshia kwa kutibu upotevu wa nywele) na minoksidili.

Uchunguzi unaonyesha kupungua kwa testosteroni bure pamoja na kuongezeka kwa nguvu kutokana na mafunzo(yasiyobainika)ya utaratibu wa nguvu.

Kupunguza mfadhaiko

hariri

Kupunguza mfadhaiko kunaweza kusaidia kupunguza kasi ya upotevu wa nywele.

Vizuiakinga-mwili

hariri

Vizuiakinga-mwili vinavyotumiwa kichwani zimeonyeshwa kugeuza kwa muda alopeshia areata, ingawa madhara ya baadhi ya dawa hizi husababisha maswala kuzushwa kuhusu dawa hizi.[18][19]

Kuficha potevu wa nywele

hariri

Kichwa

hariri

Njia moja ya kuficha upotevu wa nywele ni mtindo wa kuchana "kufunika", ambapo nywele zilizosalia hutengenezwa kwa mkao wa kufidia eneo la upara. Hii aghalabu huwa suluhisho la muda, na hufidia tu iwapo eneo lililipoteza nywele ni ndogo. Jinsi upotevu wa nywele huongezeka , kuchana "kufunika" hauweza tena kutegemewa. Wakati hali hii hufikia hatua ya juhudi kubwa na manufaa madogo-inaweza kumfanya mtu kukejeliwa au kudharauliwa.

Njia nyingine ni ya kuvaa kofia au kibandiko cha nywele- wigi au nywele za bandia. Wigi ni safu ya nywele bandia au halisi ambazo kwa kawaida hutengezwa kwa mitindo inayofanana na nywele za kawaida. Mara nyingi nywele hizi ni bandia. Wigi hutofautiana sana katika ubora na gharama. Nchini Marekani, wigi bora zaidi-ni zile zinazofanana na nywele halisi-hugharimu hadi kumi ya maelfu ya dola. Mashirika pia hukusanya 'michango ya nywele asili za watu binafsi ili kutengenezea wigi kwa wagonjwa wachanga wa saratani yaambao wamepoteza nywele zao kutokana na kemotherapia au matibabu mengine ya kansa mbali na aina yoyote ya upotevu wa nywele.

Ikumbukwe kuwa idadi kadhaa ya vibandiko maarurufu mbadala vipo kama vile Nanogen (Uropa) na Toppik (Marekani) nazo ni maarufu sana kama vipodozi visivyo vya wigi ambavyo huchangia unyuzi-embamba wa elektrostati kwa nywele za mtu binafsi.

Ingawa si kawaida kama vile upotevu wa nywele kichwani, kemotherapia, kutosawazika kwa homoni, aina za alopeshia, na sababu nyinginezo zinaweza pia kusababisha upotevu wa nywele katika nyusi. Nyusi bandia hupatikana kufidia nyusi zisizokuwepo au kufunika nyusi zenye mianya. Uchoraji mdogo sana wa kuchanja pia huwezekana.

Kukubali upara

hariri

Badala ya kuficha upotevu wa nywele, mtu anaweza kuikubali hali hiyo. Kichwa kilichonyolewa huotesha vishina kwa namna na kiwango sawa na unyoaji wa nywele za usoni. Umma kwa jumla umeweza kukubali unyoaji wa kichwa pia, lakini upara wa wanawake bado haujakubalika sana kijamii.

Jamii na utamaduni

hariri

Pana visasili vingi kuhusiana na sababu za upara na ulingano wazo na nguvu za kiumeza mtu, uwerevu wake, kabila, kazi, tabaka la kijamii, utajiri n.k. Ingawa kutia shaka kunatarajiwa kutokana na ukosefu wa ithibati za kisayansi, baadhi ya visasili hivi vina kiwango cha ukweli wa kimsingi .

  • "Unarithi upara kutoka kwa baba ya mama yako."
    • Hapo awali, upara wa mapema wa aina ya androjeni ilidhaniwa kuhusiana na hali-ngono zilizolizoshamiri katika wanaume na kwa kufifia hali-ngono katika wanawake.
    • Utafiti unaonyesha kwamba jeni kwa vipokezi androjeni, ambayo ni muhimu katika kuamua uwezekano wa kupoteza nywele, ipo kwenye kromosomu X na hivyo daima hurithiwa kutoka upande wa mama.[20] Pana uwezekano wa 50% kwamba mtu huwa na kromosomu X sawa na babuye wa kuukeni. Kwa vile wanawake wana kromosomu X mbili, wao huwa na nakala mbili za jeni pokezi ya androjeni ilhali wanaume wana moja tu. Hata hivyo, utafiti pia unaonyesha kuwa mtu aliye na baba mwenye upara pia ana nafasi kubwa sana ya kukumbwa na upotevu wa nywele.[21]
  • "Shughuli za ubongo au matatizo ya kisaikolojia yanaweza kusababisha upara."
    • Wazo hili linaweza kutokana na sababu kuwa kolesteroli hushirikishwa katika mchakato wa neurojenesi na pia vifaa vya mkisingi ambavyo mwili hutumia kuunda DHT. Licha ya kwamba wazo kuwa watu wenye upara ni werevu zaidi huenda halina mashiko katika ulimwengu wa kisasa, katika ulimwengu wa kale kama mtu aliyekuwa na upara, iliwezekana kwamba alikuwa na kiasi cha kutosha cha mafuta katika mlo wake. Kwa hiyo, ukuaji wa akili yake labda haukudumaa kwa utapiamlo katika miaka yake muhimu ya awali, alikuwa na uwezekano mkubwa wa kuwa tajiri, na pia kuwa alipata elimu ya kimsingi. Hata hivyo, maisha ya kulazadamu na uwerevu katika ulimwengu wa kisasa, hauwezi kuhusishwa mno na hali ya ulaji mafuta unaoambatanishwa na tabaka la kiuchumi katika nchi za kisasa zilizoendelea. Uwezekano mwingine ni kwamba kwa baadhi ya watu,wakati wa kujamiana hali yao kijamii iliyoyokana na uwerevu, huweza kufidiana na upungufu wa mvutio unaoletwa na upotevu wa nywele na hivyo kuzalisha watoto wa kiume ambao hukabiliwa na hali zote mbili za uwerevu au upotevu nywele. Hata hivyo, kwa mujibu wa hali bora ya kijami na kiuchumi na hivyo uwezo zaidi wa kugharamia matibabu ya upotevu wa nywele , katika miaka ya hivi karibuni uwezekano wa kudai uhusiano baina ya uwerevu na upotevu halisi wa nywele ni mdogo. Bila shaka, mbali na sababu hizi zote za kisayansi, upara unaweza tu kuhusishwa na uwerevu au hekima kwa sababu watu hupata upara jinsi umri unavyokua na tajriba kuzidi, huku watu wenye uwerevu mdogo wakifa wangali wachanga.
    • Testosteroni nyingi hudhihirisha uhusiano chanya na uwezo wa mbinu-nyingi na uwezo usio wa kawaida. Testosteroni nyingi ina uhusiano hasi na ufasaha wa kimaongezi wa mtu. Testosteroni katika mate pia ina uhusiano chanya na uwingi-mbinu katika ufanisi wa mitihani, pamoja na, uhuru wa kitaalamu. DHT na uwiano wa DHT/testosteroni nyingi una uhusiano chanya na ufasaha wa kimaongezi na uhusiano hasi na kiwango cha uwezo usio wa kawaida na uwingi-mbinu. [22]
  • "Upara husababishwa na mfadhaiko wa hisia, usinyifu wa kingono n.k"
    • Msongo wa hisia umeonekana kuharakisha upara kwa watu wenye jeni za zinazoweza kuzua upara.[23]
    • Msongo kutokana na kutolala vya kutosha miongoni mwa makurutu wa kijeshi ulipunguza kiwango cha testosteroni, lakini haujabanika kuathiri SHBG.[24] Hivyo, mfadhaiko kutokana na kutolala vya kutosha kwa wanaume wenye afya hauna uwezekano wa kuzidisha DHT, ambayo husababisha mkondo wa upara wa kiume. Si wazi iwapo inaweza kusababisha upotevu wa nywele kwa njia nyingine ile.
  • "Wanaume wenye upara wana uwezo zaidi 'wa kiume' au kujamiiana kuliko wengine."
    • Kiwango cha testosteroni huria huhusiana kwa dhati na utashi wa ngono na pia viwango vya DHT, lakini mradi testosteroni huria hukaribia kutokuwepo haijabainika wazi jinsi inavyoathiri uwezo wa kiume. Wanaume wenye androjeni alopeshia wana uwezekano mkubwa kimsingi wa kuwa na androgeni huria. Hata hivyo, uwezo wa kingono hutokana na sababu nyingi, na sifa za androjeni sio tu ya pekee inayoamua hali ya upara. Zaidi ya hayo, kwa kuwa upotevu wa nywele ni endelevu na testosteroni huria hupungua kulingana na umri, ukanda wa nywele kichwani unaweza zaidi kuwa dalili ya siku zao za nyuma kuliko ya / sasa.[25][26]
  • "Kumwaga shahawa mara kwa mara husababisha upara"
    • Pana imani nyingi potovu kuhusu kinachoweza kusaidia kuzuia upoteaji wa nywele, mojawapo ikiwa kwamba umwagaji shahawawa mara kwa mara unaweza kuathiri MPB. Kulingana na idadi ya nyakati, inaweza kuongeza au kupunguza plazma ya testosteroni.[27]
  • "Mtu asimamapo kwa kichwa huepusha upara"
  • "Kofia zinazokaza kichwani husababisha upara."
    • Ingawa hii inaweza kuwa imani potovu, kofia husababisha kukatika kwa nywele na, kwa kiwango kidogo, kupasuka mwisho kwa nywele. Kwa kuwa kofia hazioshwi mara kwa mara kama nguo nyingine, znaweza pia kusababisha uchafu kichwani na uwezekano uchafuzi wa Pitirosporamu ovali kwa wanaume walio na ngozi ambazo kwa kawaida zina mafuta. Baadhi ya magonjwa ya kichwani, yakiachwa bila kutibiwa, yanaweza kusababisha upotevu wa nywele.

Utafiti

hariri

Utafiti unaangazia uhusiano kati ya upotevu wa nywele na masuala mengine ya afya. Ingawa pamekuwepo uvumi juu ya uhusiano kati ya kuanza mapema kwa-androjeni alopeshia na maradhi ya moyo, upitiaji upya wa makala kuanzia 1954-1999 haikupata uhusiano wa kudumu kati ya upara na ugonjwa wa mishipa ya moyo. Wataalamu wa ngozi walioendesha shughuli hiyo walipendekeza utafiti zaidi unahitajika.

Sababu za kimazingira zinachunguzwa upya. Utafiti wa mwaka 2007 ulionyesha kuwa uvutaji sigara unaweza kuwa sababu inayohusishwa na upotevu wa nywele kutokana na uzee miongoni mwa wanaume wa Kiesia. Utafiti huu uliozingatia maswala ya umri na historia ya familia, ulipa takwimu kubwa ya uhusiano chanya kati ya androjeni alopeshia kali au wastani na uvutaji sigara.[28]

Katika Mei 2007, watafiti katika Chuo Kikuu cha Pennsylvania walivumbua njia mpya ya kisayansi ambayo huenda ikatibu upara kwa seli shina. Bidhaa hii inaweza kuwa sokoni katika muda wa miaka mitatu ijayo.[29][30] Watafiti waligundua kwamba ukuaji wa shina mpya zinazoweza kuotesha nywele uliweza kusisimuliwa katika panya kwa kuharibu ngozi zao.[31]

Februari 2008 watafiti katika Chuo Kikuu cha Bonn walitangaza kugundua msingi wa kijentiki wa aina mbili tofauti ya ipotevu wa nywele uliorithiwa, hivyo basi wakafungua njia pana ya matibabu ya upara. Ukweli kwamba kipokezi mahususi kilikuwa na wajibu maalum katika ukuaji wa nywele haukujulikana awali kwa wanasayansi na kutikana na maarifa haya mapya, tafiti zinazolenga kugundua jeni zaidi za aina hii huenda ikachangia ongezeko la tiba kwa aina tofauti za upotezavu wa nywele.[32][33]

Utafiti wa miezi minane katika Taasisi ya Sayansi ya Dawa katika Chuo Kikuu cha Sayansi ya Malaysia ulionyesha virutubisho vya kila siku vilivyodhihirishwa vya tokotrienoli(vitamini E) tata inaweza kuongeza ukuaji wa nywele kwa watu wenye mkondo wa upara wa kiume kwa asilimia 42.[34]

Mnamo Mei 2009, watafiti kule Ujapani walitambua jeni, SOX21, inayoonekana kuwa ndiyo yenye wajibu wa upotevu wa nywele kwa watu.[35]

Marejeo

hariri
  1. Rebora A (2004). "Pathogenesis of androgenetic alopecia". J Am Acad Dermatol. 50 (5): 777–9. doi:10.1016/j.jaad.2003.11.073. PMID 15097964.
  2. Nnoruka E, Nnoruka N (2005). "Hair loss: is there a relationship with hair care practices in Nigeria?". Int J Dermatol. 44 (Suppl 1): 13–7. doi:10.1111/j.1365-4632.2005.02801.x. PMID 16187950. {{cite journal}}: Unknown parameter |month= ignored (help)
  3. "Anagen Effluvium". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2010-06-16. Iliwekwa mnamo 2010-06-29. {{cite web}}: Unknown parameter |dead-url= ignored (|url-status= suggested) (help)
  4. Pappas P, Kauffman C, Perfect J, Johnson P, McKinsey D, Bamberger D, Hamill R, Sharkey P, Chapman S, Sobel J (1995). "Alopecia associated with fluconazole therapy". Ann Intern Med. 123 (5): 354–7. PMID 7625624.{{cite journal}}: CS1 maint: multiple names: authors list (link)
  5. "Congenital triangular alopecia". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2011-07-13. Iliwekwa mnamo 2010-06-29.
  6. 6.0 6.1 Muscarella, F. & Cunningham, M.R. (1996). "The evolutionary significance and social perception of male pattern baldness and facial hair". Ethology and Sociobiology. 17 (2): 99–117. doi:10.1016/0162-3095(95)00130-1.{{cite journal}}: CS1 maint: multiple names: authors list (link)
  7. Henss, R. (2001). "Social perceptions of male pattern baldness. A review". Dermatology and Psychosomatics. 2 (1): 63–71. doi:10.1159/000049641.
  8. Stanley Rice (1987). "On the Problem of Apparent Evil in the Natural World". Perspectives on Science and Christian Faith. 39: 150–157. {{cite journal}}: Unknown parameter |month= ignored (help)
  9. Hillmer AM, Hanneken S, Maumbile tofauti ya jeni pokezi ya Androjeni katika binadamu ndiyo sababu kuu ya kawaida ya kuanza mapema kwa Androjeneti Alopeshia (AGA). Idara ya Genomi, Maisha na Kituo cha Ubongo, Chuo Kikuu cha Bonn, Bonn, Ujerumani.
  10. Levy-Nissenbaum E, Bar-Natan M, Thibitisho la uhusiano baina ya mkondo wa Upara wa kiume na jeni pokezi ya androjeni, Taasisi ya Gartner Danek ya Jenetiki ya Binadamu, Kituo cha Matibabu cha Sheba , Tel Hashomer, Israeli
  11. Hillmer AM, Flaquer A, Utafiti wa AGA wa Ushikamano wa Ukaguzi wa Jenomu-pana na ujenzi-ramani unadhihirisha lokaso ya kromosomu 3q26. Idara ya Jenomu, Kituo cha Maisha na Ubongo, Chuo Kikuu cha Bonn, D-53127 Bonn, Ujerumani.
  12. Petukhova L, Sousa EC Jr, Martinez-Mir A, Vitebsky A, Dos Santos LG, Shapiro L, Haynes C, Gordon D, Shimomura Y, Christiano AM. Uchambuzi wa uhusiano wa jenomu-pana kuhusu haipotrikosisi hafifu ya autosomal unabainisha mabadiliko makubwa ya P2RY5. Jenomu. 2008 Novemba, 92 (5) :273-8. Epub 2008 13 Septemba. PubMed PMID: 18692127.
  13. "Women and Hair Loss: The Causes". Iliwekwa mnamo 2010-06-29.
  14. "Female, Male Balding Not the Same Pattern". Iliwekwa mnamo 2010-06-29.
  15. "Andogenetic Alopecia". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2010-06-16. Iliwekwa mnamo 2010-06-29. {{cite web}}: Unknown parameter |dead-url= ignored (|url-status= suggested) (help)
  16. Poot F (2004). "[Psychological consequences of chronic hair diseases]". Rev Med Brux. 25 (4): A286–8. PMID 15516058.
  17. Passchier J, Erdman J, Hammiche F, Erdman R (2006). "Androgenetic alopecia: stress of discovery". Psychol Rep. 98 (1): 226–8. doi:10.2466/PR0.98.1.226-228. PMID 16673981.{{cite journal}}: CS1 maint: multiple names: authors list (link)
  18. Joly P (2006). "The use of methotrexate alone or in combination with low doses of oral corticosteroids in the treatment of alopecia totalis or universalis". J Am Acad Dermatol. 55 (4): 632–6. doi:10.1016/j.jaad.2005.09.010. PMID 17010743. {{cite journal}}: Unknown parameter |month= ignored (help)
  19. Freyschmidt-Paul P, Ziegler A, McElwee KJ; na wenz. (2001). "Treatment of alopecia areata in C3H/HeJ mice with the topical immunosuppressant FK506 (Tacrolimus)". Eur J Dermatol. 11 (5): 405–9. PMID 11525945. {{cite journal}}: Explicit use of et al. in: |author= (help)CS1 maint: multiple names: authors list (link)
  20. Hillmer A, Hanneken S, Ritzmann S, Becker T, Freudenberg J, Brockschmidt F, Flaquer A, Freudenberg-Hua Y, Jamra R, Metzen C, Heyn U, Schweiger N, Betz R, Blaumeiser B, Hampe J, Schreiber S, Schulze T, Hennies H, Schumacher J, Propping P, Ruzicka T, Cichon S, Wienker T, Kruse R, Nothen M (2005). "Genetic variation in the human androgen receptor gene is the major determinant of common early-onset androgenetic alopecia". Am J Hum Genet. 77 (1): 140–8. doi:10.1086/431425. PMC 1226186. PMID 15902657.{{cite journal}}: CS1 maint: multiple names: authors list (link)
  21. Chumlea W, Rhodes T, Girman C, Johnson-Levonas A, Lilly F, Wu R, Guo S (2004). "Family history and risk of hair loss". Dermatology. 209 (1): 33–9. doi:10.1159/000078584. PMID 15237265.{{cite journal}}: CS1 maint: multiple names: authors list (link)
  22. Christiansen K (1993). "Sex hormone-related variations of cognitive performance in !Kung San hunter-gatherers of Namibia". Neuropsychobiology. 27 (2): 97–107. doi:10.1159/000118961. PMID 8515835.
  23. Schmidt J (1994). "Hormonal basis of male and female androgenic alopecia: clinical relevance". Skin Pharmacol. 7 (1–2): 61–6. doi:10.1159/000211275. PMID 8003325.
  24. Remes K, Kuoppasalmi K, Adlercreutz H (1985). "Effect of physical exercise and sleep deprivation on plasma androgen levels: modifying effect of physical fitness". Int J Sports Med. 6 (3): 131–5. doi:10.1055/s-2008-1025825. PMID 4040893.{{cite journal}}: CS1 maint: multiple names: authors list (link)
  25. Toone B, Wheeler M, Nanjee M, Fenwick P, Grant R (1983). "Sex hormones, sexual activity and plasma anticonvulsant levels in male epileptics". J Neurol Neurosurg Psychiatry. 46 (9): 824–6. doi:10.1136/jnnp.46.9.824. PMC 1027564. PMID 6413659.{{cite journal}}: CS1 maint: multiple names: authors list (link)
  26. Davidson J, Kwan M, Greenleaf W (1982). "Hormonal replacement and sexuality in men". Clin Endocrinol Metab. 11 (3): 599–623. doi:10.1016/S0300-595X(82)80003-0. PMID 6814798.{{cite journal}}: CS1 maint: multiple names: authors list (link)
  27. Exton MS, Krüger TH, Bursch N; na wenz. (2001). "Endocrine response to masturbation-induced orgasm in healthy men following a 3-week sexual abstinence". World J Urol. 19 (5): 377–82. doi:10.1007/s003450100222. PMID 11760788. {{cite journal}}: Explicit use of et al. in: |author= (help); Unknown parameter |month= ignored (help)CS1 maint: multiple names: authors list (link)
  28. Wanaume wa Kiasia wanaovuta sigara wanaweza kuwa k ongezeko kubwa la hatari ya kupoteza nywele
    Su LH, Chen TH (2007). "Association of androgenetic alopecia with smoking and its prevalence among Asian men: a community-based survey". Arch Dermatol. 143 (11): 1401–6. doi:10.1001/archderm.143.11.1401. PMID 18025364. {{cite journal}}: Unknown parameter |month= ignored (help)
  29. [1]
  30. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2008-12-19. Iliwekwa mnamo 2021-01-17. {{cite web}}: Unknown parameter |= ignored (help); Unknown parameter |https://web.archive.org/web/20081219094737/http://video.msn.com/?mkt= ignored (help)
  31. Berman, Jessica. "Scientists Grow New Hair in Mice", VOA News, Voice of America, 17 Mei 2007. Retrieved on 5 Januari 2009. Archived from the original on 2008-12-16. 
  32. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2008-06-24. Iliwekwa mnamo 2022-01-04.
  33. [2]
  34. [3]
  35. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2009-05-30. Iliwekwa mnamo 2010-11-30.

Marejeo ya ziada

hariri
  • Cyclopaedia, London: Ephraim Chambers, 1728.
  • Rossi S (: mha.) (2004). Kitabu-elekevu cha Madawa cha Australia 2004. Adelaide: Kitabu-elekevu cha Madawa cha Australia. ISBN 0-9578521-4-2
  • Stárka L, Cermáková I, Dusková M, Hill M, Dolezal M, Polácek V (2004). "Hormonal profile of men with premature balding". Exp Clin Endocrinol Diabetes. 112 (1): 24–8. doi:10.1055/s-2004-815723. PMID 14758568.{{cite journal}}: CS1 maint: multiple names: authors list (link)

Viungo vya nje

hariri
 
Simple English Wiktionary
Wikamusi ya Kiswahili ina maelezo na tafsiri ya maana ya neno: