Berrell Jensen

Mchongaji wa Afrika Kusini
(Elekezwa kutoka Berrel Jensen)


Berrell Elizabeth Jensen (22 Machi 193325 Julai 2015[1]) alikuwa msanii wa sanaa ya uchongaji, mfanyakazi wa mambo ya kijamii na mwalimu kutoka Afrika Kusini. Anafahamika kwa kazi yake ya shaba ya kuchomea na vyuma vingine.

Berrell Elizabeth Jensen
Alizaliwa 22 Machi 1933
Alikufa 25 Julia 2015
Nchi Afrika kusini
Kazi yake Mchoraji

Mwaka 1960 aliandaa maonyesho yake ya kwanza ya sanaa za uchongaji na mwaka 1968 alihamia barani Ulaya na kufungua kituo binafsi nchini Ireland, pamoja na elimu ya watu wazima na kituo cha kijamii nchini Uingereza.

Maisha ya awali na Elimu

hariri

Jensen alizaliwa mwaka 1933 katika mji wa Potchefstroom, nchini Afrika ya Kusini. Alikuwa na kaka watatu. Jensen ni mhitimu katika Chuo kikuu cha Natal kilichopo katika jiji la Durban ambapo alipata shahada ya Sayansi ya Jamii.

Mnamo mwaka 1958 alichukua mafunzo ya uchomeleaji katika chuo cha Natal Technical College ambapo baada ya hapo alianza kutengeneza vifaa na urembo unaotokana na chuma. Mwaka 1984 Jensen alichukua astashahada ya mipango katika chuo cha Architectural Association School of Architecture katika jiji la London.[1][2]

Maisha binafsi

hariri

Mnamo mwaka 1957 Jensen aliolewa na Anton Jensen, mwanafunzi mwenye PhD, ambaye alipata naye mtoto wa kiume na wa kike. Kutokana na ubaguzi wa rangi, yeye na mume wake waliamua kuhamia Ulaya kutoka Johannesburg. Walikwama, na familia ilipata ajali ya gari mnamo mwaka 1969 ambapo ndipo mume wake Jensen alifariki dunia. Jensen na watoto wake walibaki Ugiriki na kwa kipindi kifupi kuhamia Uingereza, na pia, mwaka 1977, walifika ''County Donegal'', Ireland, wakati alialikwa na padre wa kasisi ya kijamii James McDyer kuanzisha kituo cha sanaa na ufundi. Jensen baadae aliishi Belfast na hatimae London ambapo alifanya lazi kwenye huduma za jamii, alianzisha na kuendesha kituo cha elimu ya watu wazima na kituo cha jamii pamoja na Archway, London, Highgate na Hampstead. Alistaafu kazi Ireland, lakini aliendelea kufanya kazi kama mchongaji.[1][2][3][4]

Marejeo

hariri
  1. 1.0 1.1 1.2 "Obituaries – Berrell Jensen". Architectural Association School of Architecture. Iliwekwa mnamo 29 Machi 2020.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) CS1 maint: url-status (link)
  2. 2.0 2.1 "Hands-on Berrell got community centre out of a fix". Camden New Journal. Iliwekwa mnamo 29 Machi 2020.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. "New angle on Berrell's art", 2 March 1972. 
  4. "Berrell JENSEN archives". art-archives-southafrica.ch. Iliwekwa mnamo 29 Machi 2020.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Berrell Jensen kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.