Córdoba, Hispania

Cordoba (kwa Kihispania: Córdoba, tamka kor-do-ba) ni mji wa kihistoria wa Andalusia kusini mwa Hispania kando ya mto Guadalquivir. Ni makao makuu ya mkoa wa Cordoba. Kuna wakazi 321,000.

Kitovu cha kihistoria cha Cordoba pamoja na mesqita.
Ndani ya Mesqita ya Cordoba.

Historia

hariri

Kwa jina la Corduba ulikuwa mji mkubwa wa Hispania kusini wakati wa Dola la Roma.

Tangu karne ya 3 ulikuwa makao ya askofu. Askofu Ossius wa Corduba alishiriki katika Mtaguso wa kwanza wa Nisea (325).

Baadaye mji ulikuwa sehemu ya falme za Wavisigothi na Bizanti.

Mwaka 711 ulivamiwa na Waarabu Waislamu ukawa mji mkuu wa utemi na baadaye Ukhalifa wa Wamuawiya wa Cordoba. Wakati wa ukhalifa mji ukaitwa Qurtuba (kwa Kiarabu 'قرطبة') na ulikuwa na wakazi nusu milioni: ulikuwa kati ya miji mikubwa duniani ya karne hiyo. Wakazi walikuwa mchanganyiko wa Wakristo, Waislamu na Wayahudi.

Baada ya mwisho wa ukhalifa wa Cordoba mji ulivamiwa na majirani mbalimbali ukawa chini ya utawala wa Waabadiya wa Sevilla, tangu mwaka 1069 chini ya Wamurabitun kutoka Moroko na Wamuwahidun.

Mwaka 1236 jeshi la Wakristo kutoka Hispania kaskazini likateka mji ukabaki chini ya utawala wao na kuwa sehemu ya Hispania ya Kikristo.

Kati ya majengo ya kihistoria kuna

  1. Daraja la Kiroma lilijengwa na Waroma wa Kale mwaka 45 likatengenezwa na kuimarishwa na Waarabu na Wahispania.
  2. Mezquita de Cordoba iliyoanzishwa mwaka 785 na Emir Abd ar Rahman kama msikiti uliopanuliwa mara kadhaa hadi kufunika eneo la 23,000. Mwaka 1236 ilibadilishwa kuwa kanisa kuu la mji. Pamoja na majengo mengine yamepokewa katika orodha ya urithi wa dunia ya UNESCO.
  Makala hii kuhusu maeneo ya Hispania bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Córdoba, Hispania kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.