Nafaka

(Elekezwa kutoka Cereal)

Nafaka ni mbegu za aina mbalimbali za manyasi. Ni pia jina la aina za manyasi yanayolimwa mashambani ambazo mbegu zake zinatumiwa kama chakula cha binadamu.

Vyakula vinavyotokana na nafaka.

Manyasi za nafaka ni kati ya mimea muhimu zaidi inayotumiwa kama chakula cha watu duniani.

Nafaka muhimu ni pamoja na

Aina tatu za nafaka, ambazo ni 87 % za mavuno ya nafaka zote duniani, ni: mahindi, ngano na mchele.

Nafaka zina wanga (kabohaidreti) ndani yake ambayo ni lishe muhimu ya watu. Kuna pia kiasi kidogo cha protini.

Punje za nafaka zinaliwa baada ya kuzivunja kiasi na kuzilainisha ndani ya maji. Kwa kawaida nafaka huliwa baada ya kupondwa au kusagwa kuwa unga.

Ugali, uji, maandazi, chapati, mkate, keki na spaghetti ni mifano ya vyakula vinavyotengenezwa kwa kutumia unga wa nafaka.

Marejeo

hariri
  1. msamiati wa Legere kwa Roggen / rye; TUKI-ESD inataja shayiri kuwa "barley" na pia na "oat""rye"
  2. Kiing. barley
  3. msamiati wa Legere kwa Hafer / oat; TUKI-ESD inataja shayiri kuwa "barley" na pia na "oat""rye"

Viungo vya nje

hariri
 
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  Makala hii kuhusu mambo ya biolojia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Nafaka kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.