Charles Martial Lavigerie (1825-1892) alikuwa askofu mkuu wa Algiers, Aljeria, na kardinali wa Kanisa Katoliki.

Kardinali Lavigerie, mwanzilishi wa shirika la kimisionari la White Fathers.

Ni maarufu hasa kwa kuanzisha mwaka 1868 shirika la Wamisionari wa Bibi Yetu wa Afrika (kifupi: Wamisionari wa Afrika, M. Afr.) linalojulikana kwa Kiingereza kama "White Fathers" (kwa Kifaransa "Pères Blancs"), kutokana na rangi ya kanzu yao.

Lengo lilikuwa hasa uinjilishaji wa bara la Afrika, na kweli wanashirika walijitosa kufanya kazi kubwa ambayo inaendelea hata leo, ambapo lina mapadri kama 1,500.

Kisheria ni shirika la maisha ya kitume. Wanashirika hawaweki nadhiri kama watawa, ila kiapo cha kufanya umisionari kwa Waafrika hadi kifo chao.

Kwa agizo la mwanzilishi wao wanatakiwa kuishi katika jumuia yenye wamisionari kutoka nchi mbalimbali na kutumia hata kati yao lugha ya wenyeji.

Barua yake ya mwaka 1886 kwa Papa Leo XIII inasema: "Wao wanataka utawala, utaalamu na uchumi. Sisi basi, tujitahidi kuleta Ukristo na uhuru wa kweli. Afrika iwe nchi ya Waafrika, nao Waafrika wasigeuzwe kuwa Wazungu weusi." [1].

Tanbihi hariri

  1. Kanisa katika Tanzania, V2, Kitabu cha Mwalimu, Ndanda Mission Press, 1975, uk.17.

Viungo vya nje hariri

  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.