Daudi Lewis
Daudi Lewis, S.J. (Abergavenny, Monmouthshire, Welisi, 1616 - Usk 27 Agosti 1679), alikuwa padri Mjesuiti aliyefanya uchungaji kwa siri muda wa miaka 30 huko Welisi (Ufalme wa Muungano)[1].
Mtoto wa kasisi wa Anglikana, aliongokea Kanisa Katoliki huko Paris (Ufaransa) akasomea upadri huko Roma (Italia). Miaka mitatu baada ya kupadrishwa mwaka 1642 alijiunga na Shirika la Yesu.
Hatimaye alifia imani yake kutokana na dhuluma ya mfalme Charles II[2].
Anaheshimiwa na Kanisa Katoliki kama mtakatifu mfiadini. Kwanza alitangazwa mwenye heri na Papa Pius XI mwaka 1929, halafu mtakatifu na Papa Paulo VI tarehe 25 Oktoba 1970.
Tazama pia
haririTanbihi
hariri- ↑ https://www.santiebeati.it/dettaglio/93227
- ↑ Maneno yake ya mwishomwisho yalikuwa:My religion is Roman Catholic; in it I have loved above these forty years; in it now I die, and so fixedly die, that if all the good things in the world were offered to me to renounce it, all should not remove me one hair’s breadth from the Roman Catholic faith. A Roman Catholic I am; a Roman Catholic priest I am; a Roman Catholic priest of that order known as the Society of Jesus, I am;"
- ↑ Martyrologium Romanum
Vyanzo
hariri- Herbermann, Charles, ed (1913). "Ven. Charles Baker". Catholic Encyclopedia. Robert Appleton Company.
- Jones, Gareth A. (1999). In Thoroughgoing Service: The Life of Saint David Lewis. Archdiocese of Cardiff. Iliwekwa mnamo 2014-07-12.
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |