Fransisko Solano

Fransisko Solano, O.F.M. (jina la Kihispania kwa kirefu lilikuwa: Francisco Sánchez-Solano Jiménez; Montilla, Córdoba, 10 Machi 1549 - Lima, 14 Julai 1610) alikuwa mtawa wa urekebisho wa Wareformati wa shirika la Ndugu Wadogo na padri wa Kanisa Katoliki kutoka Hispania alifanya umisionari katika nchi mbalimbali za Amerika Kusini na hatimaye kufariki katika mji mkuu wa Peru ya leo.

Mt. Fransisko Solano alivyochorwa na mtu asiyejulikana akiwa pamoja na mwananchi wa Tucuman mwaka 1588 hivi. Miguuni pake ala ya muziki aliyoitumia kwa kawaida katika uinjilishaji.
Mt. Fransisko Solano na fahali kadiri ya Murillo.

Papa Klementi X alimtangaza mwenye heri tarehe 20 Juni 1675, halafu Papa Benedikto XIII alimtangaza mtakatifu tarehe 27 Desemba 1726.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 14 Julai[1].

Sala yakeEdit

Yesu mwema, mkombozi na rafiki yangu!

Nina kitu gani usichonipa wewe? Najua nini usiyonifundisha wewe?

Nina thamani gani usipokuwa nami?...

Ndiwe uliyeniumba, tena bila ya kuniuliza. Wewe umeniumba.

Elekeza macho yako kwangu, Bwana, na unihurumie, kwa kuwa mimi ni mkiwa na maskini...

Kwa nini, Bwana Yesu wangu, wewe umesulubiwa, nami nasaidiwa na watumishi wako?

Kwa nini wewe uchi, nami nina vazi?

Kwa nini wewe umepigwa makofi na kutiwa taji la miba, nami nimepewa vitu vyema na kufarijiwa na fadhili nyingi?...

Mungu wa roho yangu, utukuzwe kwa yale uliyonijalia!

Bwana wangu, nafurahi kwamba u Mungu; jinsi hilo lilivyo zuri!

Tazama piaEdit

TanbihiEdit

Viungo vya njeEdit

  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.