Haki za binadamu nchini Kenya
Haki za binadamu nchini Kenya ni bora kuliko katika sehemu nyingi za Afrika, ingawa bado uhuru wa kisiasa unahujumiwa.
Jamhuri ya Kenya |
Makala hii imepangwa kwa mfululizo: |
|
Nchi zingine · Atlasi |
Serikali ya Mwai Kibaki imefanya kazi kuboresha mazingira ya haki za binadamu nchini Kenya na kwa kiasi kikubwa imepunguza matumizi ya mfumo wa kisheria kuwanyanyasa wakosoaji wa serikali. Utawala wa Daniel Arap Moi ulipokea mfululizo wa ukosoaji wa kimataifa kwa rekodi yake ya haki za binadamu. Chini ya Moi, vikosi vya usalama mara kwa mara viliwapitisha viongozi wa upinzani na wanaharakati wa kupigania demokrasia hali ya kufungwa kiholela, kuwekwa kizuizini bila kesi, dhuluma wakiwa kizuizini, na kutumia nguvu za kusababisha majeraha. Wafadhili wa kimataifa na serikali kama vile za Marekani, Ujerumani, Uingereza, na Norway mara kwa mara zilivunja mahusiano ya kidiplomasia mbali na kusimamishwa misaada ya fedha, zikisubiri uboreshaji wa haki za binadamu. Chini ya serikali mpya, ukiukwaji wa haki za binadamu unaopelekewa na siasa umepunguka, lakini njia zingine za ukiukaji wa haki za binadamu zinaendelea, nyingi kwa ukubwa kwenye mikono ya vikosi vya usalama, hususani polisi. Kikosi cha polisi kwa upana kuwa kipengele fisadi zaidi nchini, hasa kwa kuchukua rushwa, kushiriki katika shughuli za uhalifu, na kutumia nguvu kupindukia dhidi ya watuhumiwa wa uhalifu na makundi ya watu. Polisi wengi ambao hutenda dhuluma bado hufanya hivyo kwa kutokujali. Hali ya magereza imebaki kuwa ya kutishia maisha. Mbali na dhuluma kwenye mikono ya polisi na katika mfumo wa utaratibu wa mashitaka, ukandamizaji wa haki katika mwenendo wa kesi za kisheria umeenea, licha ya shinikizo za hivi karibuni kwa wafanyakazi wa mahakama. Uhuru wa kusema na wa vyombo vya habari unaendelea kuathirika kupitia njia mbalimbali za unyanyasaji wa waandishi wa habari na wanaharakati. Vurugu na ubaguzi dhidi ya wanawake umekithiri. Unyanyasaji wa watoto, ikiwa ni pamoja na kufanyishwa kazi kwa kulazimishwa na ukahaba, ni tatizo kubwa. Tohara kwa wanawake (FGM) inabakia kuenea, licha ya sheria dhidi yake katika mwaka wa 2001 kwa wasichana chini ya miaka 16. Unyanyasaji wa wanawake na wasichana, ikiwa ni pamoja na ndoa mapema na urithi wa wake, ni sababu moja katika kuenea kwa virusi vya kukosa kinga katika binadamu / upungufu wa kinga mwilini unaotwaliwa UKIMWI (VVU/AIDS). Kenya ilipiga hatua kidogo ya mafanikio katika mwaka wa 2003, wakati wa ilianzisha Tumeya Kitaifa ya Haki za Binadamu, ikiwa na jukumu la kuhakikisha kuwa Kenya inafikia viwango vya kimataifa vya haki za binadamu. Pia, bunge lilipitisha Sheria ya Watoto kuhakikisha ulinzi wa watoto, vilevile Sheria ya Ulemavu, ikipiga marufuku ubaguzi dhidi ya walemavu.
Mnamo Novemba 2005 serikali ya Kenya ilipiga marufuku mikutano ya kampeni ya vyama vya upinzani, ikikataa wito kwa uchaguzi mpya. Makamu wa Rais Moody Awori alisema:
- Serikali inachukulia wito wa mikutano ya kampeni kuwa haifai na ni tisho kwa usalama wa taifa [...]
- Serikalihaitaruhusu mikutano ya kampeni na wananchi (raia) wamnaonywa kutohudhuria mikutano hii.
Tazama pia
haririMarejeo
haririViungo vya nje
hariri- Ripoti ya 2004 ya Haki za Binadamu nchini Kenya - Idara ya Marekani ya Majimbo
- Uhuru wa kujieleza nchini Kenya Ilihifadhiwa 14 Machi 2007 kwenye Wayback Machine. - IFEX
- Uwazi wa Kimataifa - Kenya Ilihifadhiwa 30 Juni 2007 kwenye Wayback Machine.
Makala hii kuhusu mambo ya sheria bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Haki za binadamu nchini Kenya kama historia yake au uhusiano wake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |