Historia ya Shelisheli

Historia ya Shelisheli inahusu funguvisiwa vya Bahari ya Hindi kati ya Afrika Mashariki na Bara Hindi ambavyo wakazi wake leo wanaunda Jamhuri ya Shelisheli.

Hakuna hakika kuhusu wakazi wa kwanza. Inaaminika ya kwamba ndio mabaharia na wafanyabiashara Waarabu.

Taarifa ya kwanza imepatikana kutoka kwa Wareno waliozunguka hapa kuanzia mwaka 1505.

Kwa karne moja na nusu meli au jahazi zilipitia Shelisheli tu kwa kusudi la kuchota maji ya kunywa au kukusanya matunda bila ya kuanzisha makao ya kudumu. Majambazi wa baharini walipenda kujificha Shelisheli.

Ndio Ufaransa uliojenga vituo vya kwanza vya kudumu mwaka 1756. Wafaransa waliita visiva "Seychelles" kwa heshima ya waziri wao wa siku zile Jean Moreau de Sechelles.

Walowezi wao walianzisha mashamba makubwa ya mazao ya biashara wakitumia watumwa kutoka Madagaska na Afrika bara kwa ajili ya kazi yenyewe.

Tangu mwaka 1814 visiwa vilikuwa chini ya Uingereza. Waingereza walivumilia walowezi na utamaduni wa Kifaransa visiwani.

Kwanza Shelisheli zilikuwa zikitawaliwa pamoja na Mauritius, lakini mwaka 1903 visiwa vilipewa cheo cha koloni mbali na Mauritius.

Mwaka 1970 Shelisheli ilipata uhuru. Katiba ya kwanza ilifuata mfano wa Uingereza lakini mwaka 1979 katiba mpya ilileta mfumo wa chama kimoja.

Tangu 1993 katiba ilisahihishwa tena ikiruhusu vyama vingi vya kisiasa. Chama kilichopata kura nyingi ndicho SPPF (Seychelles People's Progressive Front).

Tarehe 27 Februari 2019, Albert René, Rais wa Shelisheli kutoka 1977 hadi 2004 alikufa akiwa na umri wa miaka 83.

Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Historia ya Shelisheli kama enzi zake au matokeo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.