Historia ya Uislamu

Historia ya Uislamu kadiri ya wafuasi wa dini hiyo haikuanza na Mtume Muhammad kama wanavyofikiria watu wengi bali imeanza tangu alipoletwa nabii wa kwanza ulimwenguni, ambaye kwa mujibu wa Waislamu ni Nabii Adamu alipoteremshwa ulimwenguni na kupewa mwongozo na Mwenyezi Mungu wa namna gani kuishi hapa duniani kwa njia nzuri ya wema na hisani kwa kushikamana na mafunzo yake Mwenyezi Mungu na kujiepusha na makatazo yake.

Sehemu ya mfululizo wa makala juu ya

Uislamu

Imani na ibada zake

Umoja wa Mungu
Manabii
Misahafu
Malaika
Uteule
Kiyama
Nguzo za Kiislamu
ShahadaSwalaSaumu
HijaZaka

Waislamu muhimu

Muhammad

Abu BakrAli
Ukoo wa Muhammad
Maswahaba wa Muhammad
Mitume na Manabii katika Uislamu

Maandiko na Sheria

Qur'anSunnahHadithi
Wasifu wa Muhammad
Sharia
Elimu ya Sheria za KiislamuKalam

Historia ya Uislamu

Historia
SunniShi'aKharijiyaRashidunUkhalifaMaimamu

Tamaduni za Kiislamu

ShuleMadrasa
TauhidiFalsafaMaadili
Sayansi
SanaaUjenziMiji
KalendaSikukuu
Wanawake
ViongoziSiasa
Uchumi
UmmaItikadi mpyaSufii

Tazama pia

Uislamu na dini nyingine
Hofu ya Uislamu

Masimulizi ya historia hii ya Uislamu yameelezwa katika vitabu vitakatifu vya Mitume mbali mbali waliokuja duniani na kadhalika katika Qurani Tukufu. Umma mbali mbali zilizopita huko nyuma zimetajwa katika Qurani na kuelezwa namna gani zilivyoangamizwa kwa kutokubali ujumbe wa Mwenyezi Mungu na kuwakataa Mitume yake nao wakaletewa adhabu kali ya upepo au mvua au mafuriko na kadhalika.

Inasemekana katika historia ya Uislamu kuwa Mwenyezi Mungu alileta Mitume na Manabii kiasi cha 124,000 kwa ajili ya kuwaongoza binadamu kutokana na giza la ujinga na ujahili na utumwa wa kuabudu miungu mingi kuwatia kwenye nuru na mwangaza wa elimu na maarifa na ujuzi wa kumjua Mwenyezi Mungu wao aliyewaumba na kuwafanya wawakilishi wake hapa duniani. Mitume hawa na Manabii waliletwa na Mola wao kuwafahamisha wanadamu ukweli na haki iko wapi na wengine katika wao wakapewa vitabu ili wawaongoze wenziwao katika wanadamu kuwaelekeza kwenye njia ya haki.

Visa vya Mitume na Manabii hawa vinatueleza mengi kuhusu hawa wajumbe watukufu wa Mwenyezi Mungu na kuwa wote walitumwa na Mola wao kutangaza Umoja na Upweke wa Mwenyezi Mungu na kuwa Yeye hana mshirika na pekee ndiye mwenye kustahiki kuabudiwa kwa haki asishirikishwe na chochote au yeyote katika viumbe vyake wakiwa ni binadamu wenziwao au mizimu au majini au wanyama au vyenginevyo katika viumbe vyake.

Zama za Adam hadi Isa

hariri

Historia ya Uislamu imegawanyika zama mbili kubwa. Moja ni tangu alipoletwa Nabii Adam ulimwenguni mpaka alipoletwa Nabii Isa, na muda huu ni muda ambao Mwenyezi Mungu alikuwa akileta Mitume na Manabii kwa watu fulani na makabila fulani na ujumbe wake ulikuwa wakati huu kwa watu maalumu tu si kwa wanadamu wote kama inavyoeleza dini ya Uislamu. Zama za pili za historia ya Uislamu zinaanza tangu alipoletwa Muhammad mpaka siku ya Kiyama.

Zama za Mtume Muhammad mpaka siku ya Malipo

hariri

Historia ya Uislamu baada ya kuletwa Mtume Muhammad ilibadilika sana hasa baada ya Waislamu kuenea sehemu zote za duniani. Nao muda huu wa historia ya Uislamu umegawanyika sehemu mbali mbali. Kwa ufupi, zama zifuatazo ndizo zinazozungumzia historia ya Uislamu:

1- Maisha ya Muhammad - Tangu kuzaliwa kwa Mtume Muhammad mpaka kufa kwake. 2- Makhalifa Waongofu - Tangu aliposhika ukhalifa Abubakar mpaka alipouliwa Ali bin Abi Talib 3- Ukhalifa wa Bani Umayya 4- Ukhalifa wa Bani Abbas 5- Ukhalifa wa Wafatimi 6- Salajiqa 7- Vita vya Misalaba 8- Mamaliki 9- Hujuma za Wamongoli 10-Ukhalifa wa Maothmani - mpaka 1924 11-Utawala wa Wazungu 12-Kupata uhuru dola za kiislamu 13-Historia ya Uislamu mamboleo

Hata hivyo wanahistoria wengi wanaona dini hiyo imeanzishwa na Khalifa Abd Al-Maliki[1] Hatukuti maneno kama Uislamu, na Makka kabla ya karne ya nane. Wanahistoria wanaendelea kufanya utafiti kwa sababu hadithi kama za Muhammad al-Bukhari Imam Muslim na wengine hawakuandika chochote hadi karne ya 9. Kwa hiyo hawakuweza kumwona Mtume Muhammad wala mtu aliyemwona.

Marejeo

hariri
  1. "Mwanzo wa Uislamu - Uchambuzi wa Kihistoria - YouTube". www.youtube.com. Iliwekwa mnamo 2022-06-13.

Viungo vya nje

hariri