Shahada (Uislamu)
Shahada ni ungamo wa imani ya Kiislamu.
Sehemu ya mfululizo wa makala juu ya |
Imani na ibada zake |
Umoja wa Mungu |
Waislamu muhimu |
Abu Bakr • Ali |
Maandiko na Sheria |
Qur'an • Sunnah • Hadithi |
Historia ya Uislamu |
Historia |
Tamaduni za Kiislamu |
Shule • Madrasa |
Tazama pia |
Tamko hili lina maneno yafuatayo: لا إله إلا الله محمد رسول الله (Lā ilāhā illā-llāhu; muhammadun rasūlu-llāhi). Maana yake ni: "Hakuna mungu ila Allah; Muhammad ni mtume wa Allah". Katika sala maneno haya huanzishwa kwa "أشهد أن" (ash-hadu an yaani: Nakiri kwamba...).
Kwa maneno haya Mwislamu hutamka kuwa
- Mungu (Allah) ni mmoja tu hakuna mwingine
- Muhammad ni mtume na rasul wake wa mwisho.
Shahada ni moja ya nguzo tano za Uislamu. Hurudiwa kila siku na Mwislamu akifuata wajibu wake wa sala.
Kuna Washia kadhaa wanaoongeza maneno "Alīyun wali Allah" (علي ولي الله - "Ali rafiki yake Mungu") wakitaka kukiri ya kwamba katika imani yao Ali ni kiongozi teule wa Waislamu.
Kutamka shahada kwa imani ni tendo la kujiunga na Uislamu na kuwa Mwislamu.
Historia
Mfano wa kale wa shahada uko kwenye maandiko yaliyopo kwenye ukuta wa nje wa msikiti wa Kubba ya Mwamba mjini Yerusalemu uliojengwa kwa amri ya khalifa Abd al-Malik ibn Marwan mnamo mwaka 691. Hapa ina umbo lifuatalo: لا اله إلا الله وحده لا شريك له محمد رسول الله / la ilaha ila allahu wahdahu la sharika la-hu Muhammadun rasulu ʾllah(i) /„Hakuna mungu ila Allah peke, hana mwenzake, Muhammad ni mtume wa Allah". Sehemu yenye maneno yasiyotazamiwa leo kuwa sehemu ya shahada "lā šarīka la-hu" ni kutoka Kurani sura 6, 163.
Umbo jinsi nilivyo leo ni mapatano kati ya madhehebu ya Kisunni.
Matumizi ya kisiasa
Kuna bendera ya nchi kadhaa zinazoonyesha shahada:
- Bendera ya Uarabuni wa Saudia
- Somaliland
- Afghanistan kama dola ya Kiislami kati ya 1990-1992, na tena 1997 hadi 2001 chini ya serilkali ya Taliban.
- serikali ya mahakama za Kiislamu nchini Somalia mwaka 2005/2006
- chama cha Hamas kinachotawala kanda la Gaza nchini Palestina kinatumia shahada vilevile kwenye bendera