Historia ya madeni
Historia ya madeni ni rekodi ya mkopaji juu ya ulipaji wake wa madeni.[1] Ripoti hii hutokana na rekodi ya historia ya mikopo ya akopaye kutoka vyanzo mbalimbali kama vile mabenki, makampuni ya kadi karadha, mashirika ya ukusanyaji wa madeni na serikali, na jinsi anavyolipa au kuacha kulipa. [2].. Alama ya mikopo ya wakopaji ni matokeo ya mahesabu yanayotumika kutabiri tabia ya mkopaji wakati ujao.
Utaratibu huu ni wa kawaida kwenye nchi zilizoendelea. Hata hivyo katika miaka ya karibuni, nchi zinazoendelea kama vile nchi za Afrika za Kenya, Tanzania, Zambia, Ghana, Afrika Kusini, n.k. zimeingiza mfumo huo katika uchumi wake.
Katika nchi nyingi, wakati mteja anajaza maombi ya mkopo kutoka kwa benki, kampuni ya kadi ya mkopo, au duka, maelezo yao hutumwa kwa ofisi ya madeni. Ofisi ya mikopo inafananisha jina, anwani na maelezo mengine ya mwombaji wa mikopo na maelezo yaliyohifadhiwa na ofisi hiyo.
Rekodi hizi zilizokusanywa zinatumiwa na wakopeshaji kujua rekodi na uwezo wa mkopaji kulipa madeni. Nia ya kulipa madeni huonyeshwa kwa jinsi malipo ya huko nyuma yalivyolipwa. Wafanyabiashara wanapenda kuona madeni ambayo hulipwa mara kwa mara na kwa wakati.
Kumekuwa na majadiliano mengi juu ya usahihi wa ripoti hizi za madeni. Kwa ujumla, washiriki wa sekta wanasisitiza kuwa ripoti hizi ni sahihi.
Hata hivyo kuna njia mbalimbali za kusahihisha makosa katika historia ya madeni. Kwa mfano, huko Marekani mtu akipinga taarifa fulani katika historia yake ya madeni, ofisi ya madeni ina siku 30 ili kuthibitisha ripoti hiyo. Zaidi ya asilimia 70 za migogoro hii hutatuliwa ndani ya siku 14, kisha mkopaji anafahamishwa juu ya matokeo ya uchunguzi.
Historia ya madeni ya wahamiaji
haririHistoria ya madeni kawaida hukaa ndani ya nchi moja. Hata ndani ya mtandao mmoja wa kadi ya madeni kama Visa au ofisi ya madeni ya kimataifa, historia ya mikopo haitumwi kati ya nchi na nchi. Kwa mfano, ikiwa mtu ameishi Kanada kwa miaka mingi na kisha kuhamia Marekani, anapoomba mikopo Marekani, anaweza kukataliwa kwa sababu ya ukosefu wa historia ya madeni nchini Marekani, hata kama alikuwa na historia nzuri ya madeni huko Kanada.
Hii humfanya mhamiaji kuishia kuanzisha historia mpya ya madeni katika nchi mpya. Kwa hiyo, ni vigumu kwa wahamiaji kupata kadi za madeni na rehani mpaka baada ya kufanya kazi katika nchi mpya na kuwa na mapato imara kwa miaka kadhaa.
Hata hivyo, kuna wafanyabiashara wengine wanaozingatia historia ya madeni kutoka nchi nyingine, lakini hii si desturi ya kawaida. Kampuni ya kadi ya madeni kama American Express inaweza kuhamisha kadi za madeni kutoka nchi moja hadi nyingine na kwa njia hii husaidia kuanzisha historia ya madeni katika nchi mpya.
Madhara
haririNchini Marekani, bima, nyumba za kupanga, mikopo na ajira zinaweza kukataliwa kulingana na kiwango hasi cha madeni. Uchunguzi unaonyesha kuwa desturi ya waajiri kutazama historia ya madeni ya waomba kazi huwazuia kuingia kwenye soko la ajira.
Hata hivyo kampuni nyingine zinatoa huduma kama ya mkopo wa siku ya malipo bila kutazama historia ya mkopaji [3] ingawa mara nyingi kampuni hizi hushutumiwa kwa kujipatia fedha toka kwa watu wa daraja la chini, walemavu, n.k.[4]
Takwimu zinaonyesha kuwa huko Marekani mtu mmoja kati ya watu wanne wasio na kazi ni wale ambao wametakiwa kuchunguzwa historia yao ya madeni wakati wakiomba kazi. Tabia hii imekuwa ikitia wasiwasi mkubwa utawala wa Marekani. Nchini humo kuna sheria ambayo inahitaji waajiri kupata ruhusa kwanza toka kwa waomba ajira kabla ya kukusanya ripoti za historia zao za madeni.
Marejeo
hariri- ↑ Staff, Investopedia (27 Januari 2009). "Credit History - Investopedia". investopedia.com.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Credit report vs credit score
- ↑ "No teletrack loans". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2020-06-20. Iliwekwa mnamo 2018-10-01.
- ↑ "African-Americans, Renters,Divorcees Likely To Use Payday Loans", U.S. News & World Report, U.S. News & World Report, July 18, 2012.
Viungo vya nje
hariri- Jinsi ya kuweza kuishi kwenye zama za historia ya madeni
- Undani wa historia ya madeni
- Nini cha kufanya kama huna historia ya madeni?
- Jinsi ya kurekebisha historia yako ya madeni
- Ushauri wa jinsi ya kurekebisha historia yako ya madeni nchini Afrika Kusini Ilihifadhiwa 19 Oktoba 2017 kwenye Wayback Machine.
- Umuhimu wa historia ya madeni kwa wajasiriamali Afria
Makala hii kuhusu mambo ya uchumi bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Historia ya madeni kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |