Iltudi (pia: Illtyd, Eltut, Hildutus, Illtud Farchog; Ewyas Harold, Welisi, 480 hivi - Llantwit Major, Welisi, 540 hivi) alikuwa mmonaki abati anayetajwa kama mwanzilishi wa monasteri na chuo cha teolojia huko Bangor ambacho kinahesabiwa cha kwanza huko Britania[1] na, kutokana na sifa zake kubwa za utakatifu na elimu [2], kilifikia kuwa na wanafunzi zaidi ya elfu moja, ambao baadhi yao ni watakatifu kama Dewi na Samsoni wa Dol[3][4].

Mt. Iltudi katika dirisha la kioo cha rangi huko Abergavenny.

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki, Waorthodoksi na Waanglikana kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 6 Novemba[5].

Tazama pia

hariri

Tanbihi

hariri
  1. Galilee Chapel Project. "Home". Galilee Chapel Project: St. Iltud's Church, Llantwit Major. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 19 Desemba 2015. Iliwekwa mnamo 18 Februari 2014.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. http://www.santiebeati.it/dettaglio/92324
  3. Rudge, F.M. (1910). St. Illtyd. In The Catholic Encyclopedia. New York: Robert Appleton Company. Accessed 1 September 2012
  4. "St. Illtud". Lent with the Celtic Saints. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 24 Septemba 2015. Iliwekwa mnamo 19 Februari 2014.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  5. Martyrologium Romanum

Viungo vya nje

hariri
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.