John Jones
John Jones, O.F.M. (mzaliwa wa Clynnog Fawr, Caernarfonshire Gwynedd, Wales) alikuwa mtawa wa shirika la Ndugu Wadogo, padri wa Kanisa Katoliki na hatimaye mfiadini nchini Uingereza (12 Julai 1598).
Baada ya kujiunga na utawa huko Pontoise, nchini Ufaransa, kutokana na dhuluma ya serikali dhidi ya Wakatoliki, alikwenda Roma, Italia, na huko akajiunga na urekebisho wa Wariformati.
Mwaka 1591 aliomba kurudi Britania, ingawa ilijulikana kwamba hatari ya kuuawa ilikuwa kubwa. Hatimaye viongozi walikubali na Papa Klement VIII alimbariki.[1]
Kisha kufika London mwishoni mwa mwaka 1592 na kufanya utume katika sehemu mbalimbali, alichaguliwa mkuu wa kanda ya Uingereza.
Mwaka 1596, Richard Topcliffe, aliyeitwa "mwindamapadri", alimkamata na kumtesa, halafu akamuacha gerezani miaka 2.
Tarehe 3 Julai 1598 alihukumiwa adhabu ya kifo kama msaliti.
Alinyongwa hadi kufa tarehe 12 Julai mwaka huo[2]. Mabaki yake yaliangikwa katika mabarabara kabla ya kuzikwa na watu wawili, ambao mmojawao alifungwa muda mrefu kwa kufanya hivyo.
Papa Pius XI alimtangaza mwenye heri mwaka 1929, na Papa Paulo VI alimtangaza mtakatifu tarehe 25 Oktoba 1970 pamoja na wafiadini wengine 39 wa Uingereza na Wales.
Tazama pia
haririTanbihi
hariri- ↑ ""Saint John Jones", Wrexham Diocese". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2013-12-03. Iliwekwa mnamo 2014-10-05.
- ↑ https://www.santiebeati.it/dettaglio/90375
- ↑ Martyrologium Romanum
Viungo vya nje
hariri- Katika Catholic Encyclopaedia
- Historia ya Kanisa kuu la Southwark Ilihifadhiwa 1 Desemba 2005 kwenye Wayback Machine.
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |