Julian Assange
Julian Paul Assange [1] (alizaliwa Julian Paul Hawkins; 3 Julai 1971) ni mtaalamu wa kompyuta toka Australia aliye mwanzilishi na mkurugenzi wa WikiLeaks.[2]
Hivi sasa anashikiliwa na polisi London, Uingereza baada ya kukamwata tarehe 11 Aprili 2019 kwa kutotii masharti ya dhamana aliyopewa mnamo Desemba 2010. Kabla ya kukamatwa, alikuwa akiishi katika ubalozi wa Ecuador tangu mwaka 2012.
Assange alianzisha WikiLeaks mwaka 2008 akaanza kujulikana duniani mwaka 2010 wakati WikiLeaks ilipochapisha siri za serikali ya Marekani zilizofichuliwa na Chelsea Manning (akijulikana wakati huo kama Bradley Manning). Siri hizo zilijumuisha video ya Collateral Murder (Aprili 2010),[3]. Kutokana na kuchapishwa kwa siri hizo, serikali ya Marekani ilianzisha uchunguzi wa jinai na kutaka nchi marafiki kuisaidia.[4]
Marejeo
hariri- ↑ "The Julian Assange Show: Cypherpunks Uncut (p.1)" katika YouTube
- ↑ Leigh, David; Harding, Luke (2013). WikiLeaks: Inside Julian Assange's War on Secrecy. London: Faber & Faber. ISBN 9781783350186.
- ↑ Collateral Murder katika YouTube, 5 April 2000. Retrieved 28 March 2014.
- ↑ Yost, Pete. "Holder says WikiLeaks under criminal investigation", 29 November 2010. Retrieved on 15 March 2014.
Viungo vya nje
hariri- Works by Julian Assange katika Project Gutenberg
- Why Judge Baltasar Garzon has taken on the defense of Julian Assange
- Habari ya kukamatwa kwa Julian Assange toka BBC
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Julian Assange kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |