Juma (kutoka neno la Kiarabu) au wiki (kutoka Kiingereza "week") ni kipindi cha siku saba. Kila siku ina jina lake.

Katika mwaka wa kalenda ya Gregori mna majuma 52 pamoja na siku moja au mbili za ziada. Hesabu ya majuma inaendelea mfululizo bila ya kuanza upya wakati wa mwaka mpya.

Ufuatano wa majuma haulingani na mgawanyo mwingine wa wakati kwa njia ya miezi au mwaka.

Mapokeo ya Kiyahudi-Kikristo

hariri

Asili ya juma ni katika utamaduni wa kale wa Mashariki ya Kati tangu Babiloni. Imeenea duniani kote kupitia Biblia na desturi za Uyahudi na Ukristo.

Ufuatano wa siku katika mapokeo hayo huanza na Jumapili. Majina ya siku ni kama yafuatayo:

Katika mwaka juma moja la Machi mwishoni au la Aprili linaadhimishwa na Wakristo wengi kama Juma kuu, ambapo wanaadhimisha matukio makuu ya imani yao kadiri ya historia ya wokovu, yaani mateso, kifo na ufufuko wa Yesu Kristo.

Siku za Jumamosi na Jumapili mara nyingi huitwa "wikendi" (kutoka Kiingereza: "weekend", yaani mwisho wa juma). Hata hivyo katika mapokeo hayo Jumapili ni mwanzo wa wiki mpya, si mwisho wake.

Majina ya siku kwa Kiswahili

hariri

Majina ya siku tano kwa Kiswahili ni ya namba zinazoanza kuhesabiwa baada ya siku ya Ijumaa (ambayo ni siku ya sala kuu katika Uislamu): Ijumaa - Jumamosi - Jumapili - Jumatatu - Jumanne - Jumatano.

Alhamisi na Ijumaa ni majina ya lugha ya Kiarabu inayofuata mapokeo ya Kiyahudi kuhusu majina ya siku.

Hivyo "Alhamisi" ina maana ya "siku ya tano" (baada ya Jumamosi inayoitwa "sabat" kwa Kiarabu, sawa kama "shabbat" kwa Kiebrania (lugha ya Wayahudi).

"Ijumaa" ni matamshi ya Kiswahili ya jina la Kiarabu la "jum'a" inayomaanisha "siku ya mkutano" (= ya kusali pamoja).

Siku za juma (wiki)
Jumapili - Jumatatu - Jumanne - Jumatano - Alhamisi - Ijumaa - Jumamosi
  Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Juma kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.