Wikendi
Wikendi ni kipindi ambapo sehemu kubwa ya wafanyakazi katika nchi nyingi hupata nafasi ya kupumzika.
Desturi tofauti wa wikendi
haririKatika mfumo wa nchi za magharibi ni siku za Jumamosi na Jumapili. Katika nchi nyingi wa Kiislamu wikendi ni Alhamisi na Ijumaa. Katika nchi ya Israeli ni Ijumaa na Jumamosi.
Utaratibu huo haupo kwa wafanyakazi wote. Katika kilimo, hospitalini, kwenye huduma za umma kama polisi na pia kwenye mahoteli kazi inaendelea tu.
Vilevile katika nchi nyingi idadi kubwa ya watu hawana ajira wakijitegemea kwa namna fulani bila utaratibu wa saa za kazi. Hivyo katika nchi nyingi za Afrika desturi ya wikendi inahusu hasa watumishi wa serikali na makampuni makubwa.
Sabato - chanzo cha wikendi
haririMsingi wake ni amri ya dini ya Uyahudi ya kupumzika siku ya Sabato iliyochukuliwa na Wakristo wengi kama utaratibu kwa ajili ya Jumapili (wanayoiita "Dominika" yaani Siku ya Bwana kwa kuwa ndiyo siku ya ufufuko wa Yesu). Muda wa siku hii moja ya mapumziko uliongezwa katika nchi nyingi kuwa wikendi.
Desturi ilisambaa kutoka Ulaya kwa njia ya ukoloni katika nchi nyingi duniani hata kama utamaduni haukujua siku za mapumziko kama vile huko Uhindi na China.
Historia ya wikendi ya kisasa
haririDesturi ilianzishwa huko Uingereza katika karne ya 19 kama sehemu ya sheria iliyolenga kutunza afya ya wafanyakazi viwandani. Sheria iliunda utaratibu wa kuwapa nafasi ya kupumzika kuanzia Jumamosi mchana.
Nchi mbalimbali zilifuata wakati wa karne ya 20 na ofisi za serikali zilifunga pia kuanzia Jumamosi mchana. Katika nusu ya pili ya karne ya 20 muda wa mapumziko ulipanuliwa kuwa Jumamosi yote.
Siku za juma (wiki) |
---|
Jumapili - Jumatatu - Jumanne - Jumatano - Alhamisi - Ijumaa - Jumamosi |
Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Wikendi kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |