Karitoni na wenzake

(Elekezwa kutoka Karitoni, Karito na wenzao)

Karitoni na wenzake Karito, Evelpisto, Gerasi, Peoni na Liberiani (walifariki Roma, Italia, kati ya 162 na 168) walikuwa wanafunzi sita wa Yustino ambao waliuawa pamoja naye kwa kukatwa kichwa katika dhuluma ya Dola la Roma[1][2].

Picha takatifu ya Kirusi ya Mt. Yustino, mwalimu wao.

Hati za mateso yao zimetunzwa hadi leo[3].

Tangu kale wanaheshimiwa na Kanisa Katoliki, Waorthodoksi na Waorthodoksi wa Mashariki kama watakatifu wafiadini.

Sikukuu yao huadhimishwa tarehe 1 Juni[4].

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.